Afisa utumishi wa wilaya ya Kilosa - Noel Abel, awajibishwe kwa kugandamiza na kudhulumu haki za wafanyakazi wa Kilosa.

Introvet

New Member
Sep 5, 2019
1
0
Nampongeza Rais JPM kwa kazi na juhudi zake alizofanya na anazoendelea kufanya katika kusimamia uwajibikaji wa watumishi wa umma serikalini ambapo kwa sasa uwajibikaji umekuwa mkubwa, rushwa pamoja na uminywaji wa haki umepungua kwa kiasi kikubwa.

Lakini pamoja na juhudi hizo kuna baadhi ya watendaji/watumishi wa serikali ambao bado wanafanya kazi kwa mazoea, kwa kugandamiza haki za raia na wafanyakazi waliopo chini yao na kupokea hongo kwa kila kitu wanachotakiwa kufanya hata kama ni haki ya kisheria ya mtu husika.

Mojawapo ya watendaji wa serikali wanaofanya hivyo ni Afisa utumishi wa wilaya ya Kilosa, mkoa wa Morogoro, bwana Noel Abel. Huyu afisa amekuwa siku zote hafanyi kazi kwa kuzingatia taratibu na sheria zilizopo bali ni vile anavyojisia yeye. Amekuwa akiwanyima wafanyakazi waliopo chini yake haki zao za msingi miongoni mwao wakiwa ni walimu wa shule za msingi na sekondari wa halmashauri ya Kilosa. Vitu anavyovifanya bila kufuata utaratibu wa kisheria ni pamoja na kuwasimamishia mishahara walimu pasipo kupitia ngazi na hatua husika zinazotakiwa kufanywa. Kwa mfano, kama mwalimu amefanya kosa kuna hatua za kufanya kabla hujasimamisha mshahara wa mwalimu husika, hatua hizo ni Afisa utumishi akishirikiana na Afisa elimu anatakiwa kupeleka mashitaka katika Tume ya Utumishi wa Walimu (Teacher's Service Commission - TSC), tume ndio itachunguza kama hilo kosa limetendeka kweli na kumuita mwalimu husika kutoa maelezo na inapothibitika kwamba mwalimu ana kosa tume ina adhabu zake za kutoa kulingana na ukubwa wa kosa ikiwa ni onyo kwa kosa dogo kabisa na kufukuzwa kazi/kufukuzwa kazi na utumishi kwa kosa kubwa kwa mwalimu aliyefanya kosa hilo. Baada ya tume kutoa adhabu ndio sasa afisa utumishi anatakiwa kufanyia kazi maelezo ya Tume ikiwemo kumuondoa mtumishi kwenye payroll ya mishahara kama itakuwa imeamuliwa afukuzwe kazi.

Lakini kwa afisa utumishi huyu wa Kilosa yeye hafuati taratibu hizo zaidi ya kusimamisha mshahara wa mwalimu husika na hata mwalimu akidai haki yake ya kurudishiwa mshahara au kushitakiwa kwenye Tume ya utumishi wa walimu ili sheria zifuatwe, afisa utumishi huyu hupuuza na kujigamba kwa kusema kwamba hata mwalimu husika aende kwa Rais maamuzi yake ndio hayo na hawezi kufuata taratibu husika. Kuna ushahidi wa zaidi ya walimu kumi ambao wamesimamishiwa mishahara yao kwa zaidi ya miaka miwili sasa pasipo kushitakiwa TSC ili sheria iamue.

Hata Mkurugenzi wa wilaya ya Kilosa ambae ndio mwajiri wa wafanyakazi wote wa wilaya bwana Asajile Mwambambale hana la kufanya kwa ajili ya wafanyakazi wake walionyimwa haki zao ikionekana kana kwamba huyu Afisa utumishi ana nguvu kuliko hata mkurugenzi aliyepo juu yake kimadaraka na hawezi kumfanya lolote hata kama akifanya kazi kinyume na sheria.

Kutokana na hili wafanyakazi wengi wa Kilosa wamekuwa wakijiuliza;

- Je, inawezekana afisa utumishi huyu anafanya hivyo ili mfanyakazi yule aliyenyimwa haki yake aende kumpa rushwa ndipo taratibu husika zifuatwe?
- Je, inawezekana anafanya hivyo kuzuia mishahara ya wafanyakazi bila kupitia hatua husika kwa dhumuni la kuchukua yeye mwenyewe kama ambavyo ilivyokuwa inafanyika kabla ya Rais JPM kuingia madarakani ambapo baadhi ya maafisa utumishi walikuwa wanazuia mishahara ya wafanyakazi na kuingiza kwenye akaunti zao binafsi?
- Je, kama Mkurugenzi ambae ni mkubwa wake wa kazi kashindwa kumuwajibisha maanayake hakuna wa kumzuia kile anachokifanya na yuko juu ya sheria?

Kwa mtindo huo wa ufanyaji kazi wa Afisa utumishi huyu wa wilaya ya Kilosa anarudisha nyuma maendeleo ya wilaya na nchi kwa ujumla kwa kudhoofisha morali ya wafanyakazi hasa walimu kwa kudidimizwa haki zao za msingi kama taratibu na sheria zinavyotaka.

Ni vema Rais JPM na wasaidizi wake (hasa Jafo na Mkuchika) wakaliangalia na kulifuatilia swala hili kwa umakini mkubwa na kumuwajibisha afisa utumishi huyu kwa kukiuka taratibu na sheria na kuwanyima wafanyakazi wa Kilosa haki zao za msingi.

Mwanaharakati mzalendo,
Kilosa
 
Asee polen Sana walimu na watumishi wengine Ila mwambien ubabe unamwisho wake
 
watumishi wa halmashauri kwa majungu na kutunga uongo ili mchafue wenzenu hamjambo
 
Back
Top Bottom