Afisa uhamiaji mkoa wa Dar, John Msumule

Afisa uhamiaji mkoa wa Dar, John Msumule

Kwa Afisa Uhamiaji Mkoa wa DAR.
Pamoja na mapendekezo yote uliyopewa kuhusu wahamiaji na wanaofanyakazi bila vibali kuna mkenya anafahamika kwa jina la Timoth John Kamau. Yupo hapa Dar kwa miaka zaidi ya mitano kazi yake ni kutengeneza madawa ya mifugo bandia na madawa ya tiba mbadala. Hana kibali chochote anakamatwa na TFDA anahonga anatoka. Ofisi iko Mbagala.
Na babake yupo Moshi shughuli ni hizo hizo.

NATUMAINI WATAMFUATILIA...
 
Habarini wanajamvi,

Siku ya jana tarehe 14 February, 2017 tulimsikia Afisa Uhamiaji Mkuu wa Mkoa wa DSM, Ndg. John Msumule akimtaka Manji afike katika ofisi za uhamiaji kwa makosa makuu mawili, mosi kuruhusu raia wa kigeni kufanya kazi katika kampuni za Manji pasipo kuwa na vibali vya kuishi na vya kufanya hapa nchini na pili kuhojiwa juu ya uraia wa wafanyakazi wake wanaofanya kazi katika kampuni za QUALITY GROUP OF COMPANIES.

Ni jambo jema kwa kazi uliyoianza, lakini je kwa nini iwe ni Yusuph Manji na kam[uni zake za Quality Group of Companies???????

Sisi wananchi wa mkoa wa Dar es salaam, tunaamini kwamba hata katika makampuni mengine ya watanzania wazalendo pia wapo wanaofanya kazi pasipo kuwa na vibali vya kuishi au hata vya kufanya kazi, na mimi nataka sheria iwe msumeno kwa pande zote mbili, hata katika makampuni ya BAKHERESA GROUP OF COMPANIES bila kuasahau na timu yake ya AZAM, MOHAMMED ENTERPRISES, AFRICAN MEDIA GROUP, SAHARA MEDIA GROUP, IPP LTD, COCACOLA, VIWANDA VYOTE VYA MASINGASINGA NA MABOHORA HAPA MKOA WA DSM PIA WAPO WANAOISHI NA KUFANYA KAZI PASIPO KUWA NA UTARATIBU, WACHINA PALE KARIAKOO, KAMPUNI ZAUKANDARASI ZILIZOPATA TENDER HAPA NCHINI ZOTE ZA MKOA WA DSM WANAFANYA KAZI ZAO PASIPO KUWA NA VIBALI VYA KUISHI WALA VYA KUFANYA KAZI....KWAHIYO USHAURI WANGU KWAKO, ILI USIMUONEE MTU HUYU ZOEZI HILI LIWE ENDELEVU KWA KWENDA PIA KUMKAMATA NA KUMUWEKA MAHABUSU BAKHERESA, MOHAMMED DEWJI, REGINALD MENGI, WACHINA WA PALE KARIAKOO NA KAMPUNI ZAO ZA UKANDARASI, etc

Nawasilisha...!
Kamata wote tupa ndani acha ubabaishaji na unafki
 
Bila hivyo kamata afisa uhamiaji kwa makosa ya uzembe na kutafuna rushwa

NAFIKIRI HAWA WA HAPA DSM, WANAHITAJI KUHAMISHWA NA PIA KUCHUNGUZWA MALI ZAO...PCCB NA TISS MPO WAPI KUWAFUATILIA HAWA MAAFISA UHAMIAJI....I WISH I COULD BE JPM.
 
Makampuni karibu yote ya wahindi ni ya kuchunguzwa. Na maafisa uhamiaji wawajibishwe. Mhindi anaajiri accountant toka India sisi tuna CPA holder wangapi? Technical job zenyewe wabongo hawafundishwi.. Huku Mwanza waende makampuni kama Nyanza Engineering Works na Vick fish watakuta tu wageni hawana vibali.. Wanalala chumba kimoja watu 10 na kila mmoja anamiliki gari wahindi bana hawajengi ni kuiba pesa na kuwekeza India. Wafuatiliwe wote nafasi za ajira zipatikane. Na Hawa maafisa Uhamiaji wachunguzwe.
 
Sidhani kama wako kimya nafikiri na wao pia
watakuwa wanafatilia hili swala
maana hii ni baina ya nchi na nchi
Sasa endapo kama tutareact vibaya,
Tunaweza sababisha vita nafikiria wanafatilia wajue
chanzo ni nini.
Na endapo ikifahamika basi tutawataka viongozi
wa msumbiji wajibu hizi tuhuma na endapo watashindwa
tutachukua hatua nyingine.
Kwa siku hizi kadhaa zimepita serikali ilitakiwa iwe imetoa majibu ya watanzania kupigwa. [HASHTAG]#Tunataka[/HASHTAG] bunge live


wewe ni mtanzania adui kwa nchi yako. kwani umeambiwa manji yuko juu ya sheria? uhamiaji hawafanyi kazi kutokana na matakwa yako bali wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria na kulingana na taarifa walizonazo. sasa mkuu, tunaomba taarifa kuhusu hayo makampuni uliyotaja ili yafanyiwe kazi,

Brother punguza mihemko hao wahindi na waarabu wanawahonga sana uhamiahaji.. Hata ukitoa ushirikiano hawaji wanadai wao wanataratibu zao za kazi.. Rushwa tupu
 
HIVI UHAMIAJI MNASUBIRI KULETEWA TAARIFA??????? I WISH I COULD BE IMMIGRATION COMMISSIONER GENERAL...TUNASUBIRI KULETEWA TAARIFA MEZANI, BADALA YA KUZIFUATA IN THE GROUND...YAANI TUNAKAMATA WAHAMIAJI HARAMU TUKIWA MAOFISINI TUKIPIGWA NA AC'S
wewe hujaelewa dhana ya wananchi kufikisha taarifa kwenye vyombo vya dola. nani amekwambia uhamiaji wanakaa ofisini wakisubiri taarifa zako? post yangu nilimjibu mtu aliyesema kuna makampuni mengi yana wahamiaji haramu, na kwa kuwa yeye ndio anatuhumu, basi awasilishe taaarifa hizo. uwe unasoma post na kuilewa kabla ya kukurupuka
 
Back
Top Bottom