Afisa Mtendaji wa mtaa wa Mbezi Msumi ashambuliwa hadi kufa ofisini kwake

Kweli mtz mpe picha habari ataweka mwenyewe. Hata Jeshi la Polisi halijapata chanzo cha mauaji wala mtuhumiwa humu tayari upelelezi umekamilika na kubaini chanzo ni dhuluma ya viwanja, dhuluma ya haki na mapenzi. Halafu watuhumiwa ni wananchi wa mtaa huo! Mbaya zaidi mauaji yanabarikiwa na kufurahiwa sana!!

Watanzania tumefika mbali sana!

RIP mtendaji.
 
Mm hapa nawalaumu wananchi wa eneo hill niwazembe kwasababu wameshindwa kumlinda mtendaji wao.
 
Wa Tz huwa wanapenda kujidai wajuaji sana wazee wa kutoa hukumu utaskia huyo kadhulumu kiwanja au katembea na mke wa mtu, ukiuliza alidhulum nn?

Hawan majibu zaid ya kuhisi kama muuaji alikua muuza mazao hapohapo watasema alidhulum mazao
Yan akilin kwao huwa hawajui hata mtenda haki anamaadui au pia anae dhulumiwa anaweza kuuwawa
 
Dar ina watu waajabu sana unaweza kufanyiwa unyama wowote mbele ya Kadamnasi na watu wanaendelea na mambo yao tu...
Na Dar unaweza kuingilia ugomvi usiokuhusu ukauwawa wewe. Dar ni sehemu hatari sana wakati mwingine.
 
MAUAJI ya kutisha yametokea eneo la Mbezi Msumi mkoani Dar es Salaam baada ya watu wasiofahamika kudaiwa kuvamia ofisi za Serikali ya Mtaa wa eneo hilo na kisha kumuua Ofisa Mtendaji kwa kumkata na panga..
Hii issue ukifuwatilia in deep utakuta mambo ya dhuluma na issue za ardhi haya twende...
 
Baadhi ya maafisa watendaji hujihusisha na dhuluma za mambo ya kiwanja huku wakijua wamiliki halali inawezekana ikawa ndio chanjo cha unyama.
 
MAUAJI ya kutisha yametokea eneo la Mbezi Msumi mkoani Dar es Salaam baada ya watu wasiofahamika kudaiwa kuvamia ofisi za Serikali ya Mtaa wa eneo hilo na kisha kumuua Ofisa Mtendaji kwa kumkata na panga.

Tukio hilo la mauaji limetokea leo Oktoba 11, 2021 kati ya saa sita hadi saa saba mchana wa leo na inadaiwa ofisa huyo mtendaji wa Serikali ya Mtaa wa Mbezi Msumi ameshambuliwa kwa kukatwa na panga shingoni na watu ambao hawahamiki.

Akizungumza na Michuzi TV pamoja na Michuzi Blog leo Mmoja wa mashuhuda na mwananchi wa eneo hilo(jina limehifadhiwa) amedai wameshangazwa na tukio hilo la mauaji ambalo limefanywa kwa kiongozi huyo.

Alipoulizwa iwapo watu waliofanya tukio wamefahamika, amejibu hawajafahamika kwani baada ya kutekeleza unyama huo walikimbia na haijulikani ni akina nani na wametoka wapi, ingawa anaamini Jeshi la Polisi linajua namna ya kufuatilia tukio hilo na kuupata ukweli.

"Wananchi tumejawa na taharuki baada ya kutokea tukio hili la mauaji , hatuji nini kimesababisha hadi watu hao kufanya unyama huu kwa kiongozi wa Serikali ya Mtaa,tupo hapa tunasubiri kuona nini kinachoendelea,"amesema shuhuda huyo alipokuwa akizungumza na Michuzi TV

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Ramadhan Kingai aliyezungumza na Michuzi TV amethibitisha kupata taarifa hizo za tukio la mauaji na tayari askari polisi tayari wako eneo la tukio."Tumepata taarifa za tukio hilo,tunafuatilia na baadae tutatoa taaria rasmi kwa vyombo vya habari."

Michuzi TV na Michuzi Blog inaendelea kufuatilia tukio hilo kwa karibu ili kuhakikisha umma wa Watanzania unafahamu ukweli wa tukio hilo kupitia Jeshi la Polisi ambalo limeanza kufuatilia.
Pumzika kwa Amani Ba Mdogo ,Mme wa Mamdogo wangu,Umeacha Mwanao bado Mdogo na mwingine akiwa tumboni .inauma
 
Pole sana Kwake, Nimesikitika na Kuhuzunika zaidi kwani Watanzania hatujawahi kuwa na Roho za aina hii.

Hata hivyo nimalizie tu kutoa Ushauri kwa Viongozi kuwa jitahidini sana kujihusisha katika Madili ya Hatari huku mkijijua kuwa ni Wadhulumati na hamna Siri.

Pia epukeni mno Kutembea na Wake za Watu tena Kibabe na Kijeuri huku pengine hata mkiwaweka ndani Kimakusudi wenye hao Wake.

Ukijijua Wewe si Mnafiki kataa Uongozi.
 
Back
Top Bottom