Mimi ni miongoni mwa watu niliyewahi kuwa na wasiwasi kama huo. Ila amini usiamini interview zote zilizopata kufanyika mikoani mpaka leo, zote zilisimamiwa na utumishi wenyewe bila kujalisha zilifanyika kwa siku moja katika mikoa tofautitofauti. Hawa jamaa sijui wanawatumishi wangapi? Kama haitakuwa hivyo basi hii ndo itakuwa ya kwanza.
Mimi swali langu ni kwamba, kila watu wa mkoa husika watapangiwa kazi katika mkoa waliofanyia interview endapo watafaulu? au kupangiwa kituo cha kazi haitazingatia ulikofanyia interview? Maana kama itakuwa hivyo basi harufu ya ukabila na ukanda itaanza kupandwa kwa njia hii.