Afisa mstaafu wa JWTZ amiliki Tsh 50 bn nje

shida ya Zitto huwa hataji watu anaowatuhmu kwa majina anaacha kwenye dilema na hii huwa ni njia ya kukaribisha rushwa ukiwa na ushahidi wa kutosha taja jina mtu kama navofanya doctor Slaa Then mwambie aende mahakamani hujui kitu kaa kimya!
 
tusubiri tu maana yote huwa yana mwisho hata kama wanahela nje ya nchi ninaimanki tunakoelekea hawatazitumia maana nchi yetu natunakoelekea watazirudisha tu au hata kutokuzifaidi
 
Mh Zitto Kabwe amekaririwa na Gazeti la Mwananchi la 01 Okt kuwa katika yale matrilioni ya pesa zinazomilikwa na vigogo kwenye akaunti zao nje ya nchi, mmojawao ni Afisa wa JW TZ mstaafu.

Huyo mzee lazima atakuwa 60 + yrs, atazifanyia nini pesa hizo alizotuibia ktk umri huo? Anawatafutia laana tu watoto na wajukuu zake watakaorithi mapesa hayo!

Kuna kigogo mmoja wa JW TZ aliyestaafu hivi karibuni, alituhumiwa humu JF kuwa amepokea mabilioni kwa ajili ya Askari waliopo UN mission nje na kuhifadhi nje.

Habari za namna hii zinanipa kichefuchefu. Weka jina la mtu, kama huna uhakika usiweke hapa. Hatuwezi kujadili kivuli, ni mwezi uliopita tumejadili mke wa kigogo wa polisi ambaye mpaka leo hatujui ni nani.

Kama ni vigogo wastaafu wa Jeshi pia usiwasahau Lt Col Kikwete, Col Kinana, Brig Gen Ngwilizi, Capt Lowasa, Lt Makamba. Sasa tuambie kigogo yupi.
 
Ikiwa ni mara kadhaa sasa ZZT akisema atawataja waliotuibia fedha zetu na kuzificha nje bila kuwataja, nashindwa kuelewa ni nini kinamzuia kuwataja. Kusubiria eti serikali kunasiku itawashughulikia wezi hao wakati serikali ya CCM ndio mwizi ni kucheza cheusi chekundu.

Tunataka mwembe yanga sio kutishia nyau. Weka majina hadharani tuyumbe na wezi wetu kama wale wa redio na adhabu za kimila. Kama unaogopa kurushwa majina hadharani nayaomba mimi nikusaidie kuyaweka hadharani.

Chief Mkwawa wa Kalenga
Niliuwawa na wajerumani ili muishi huru

Yaani kati ya watu ambao kwa sasa sina imani nao ni ZZK. Yeye mwenyewe kwa sasa ana utajiri wa kutisha. Anatembelea Hummer, gari ambayo thamani yake ni kati ya Mil 300 na 500. Ana majumba ya kifahari. Kwa muda aliokalia ubunge haiwezekani hata kidogo kupata mali hizo. Atuambie yeye mwenyewe kapata wapi mali hizo
 
Gen Mwita Kiaro hakuwa na mapesa, Magenerali wa Mkapa na JK ndio hao mafisadi kama waliowateua.
 
Gen Mwita Kiaro hakuwa na mapesa, Magenerali wa Mkapa na JK ndio hao mafisadi kama waliowateua.

General Kiaro alikuwa muuadilifu sana...." hapana chezea Mali ya Jeshi....Chidiefu CDF...ni Chiaro..sio nyie"........alikuwa akiwaambia watoto wake...,alikataa gari la kuumbeba mkewe na mkewe alibeba kikapu kwenda sokoni pale lugalo ...CDF Resiidence Kama wake za maaskari wa chini...ambako nae alianzia....,watoto wake walipanda UDA Kama wengine......,na hata mtoto wake alipopendelewa Azania Baada ya fujo na Tambaza ....alikataa...akasema .." chimekosa chifukuzwe Kama wenzake " .... Ili kuepuka kumfukuza mtoto wa General iikabidi wote wasamehewe wwakaamishwa mashulee......msaidizi wake alikuwa Tumainiel Kiwelu yeye alikuwa msomi na msimamo wake ulikuwa Kama wa Kiaro.
 
Hii ndiyo Tanzania, wezi ni km wana kinga. Hawatajwi kwa majina yao ila kwa jina la jumla VIGOGO. Ndiyo maana manywele anasema tujifunze kuchukua maamuzi magumu.
 
Atawatajaje mashoga zake?Hilo ni vuvuzela tu, ni debe shinda.
shida ya Zitto huwa hataji watu anaowatuhmu kwa majina anaacha kwenye dilema na hii huwa ni njia ya kukaribisha rushwa ukiwa na ushahidi wa kutosha taja jina mtu kama navofanya doctor Slaa Then mwambie aende mahakamani hujui kitu kaa kimya!
 
Back
Top Bottom