Afisa maliasili aliyetukamata baada ya kugonga kanga amefariki leo

Afisa maliasili aliyetukamata baada ya kugonga kanga amefariki leo

GAZETI

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
5,292
Reaction score
6,773
Siwezi kuwa mnafiki moyo wangu umefarijika sana kwa kifo chake,

ILIKUWA HIVI;
Kuna mahali tulikuwa tunaelekea naye akiwa kwenye gari kwa bahati mzuri tukawagonga kanga wawili, kwa kuwa walikuwa wanatapatapa tukateremka na kuwahi kuwachinja na kupata kitoweo, Kumbe wakati huo mwenzetu alifanya mawasiliano na wenzake ambao walikuja na askari na kutukamata.

Sakata hilo mpaka linamalizika ilitutoka milioni moja laki mbili na elfu sabini, tukapewa maelezkezo kuwa unapomgonga mnyama au ndege wa mwituni mwache hapo hapo kuna wengine watakuja watamla.

Yaani mambo mengine ni ya ajabu sana wakati kuna waarabu wanatoka hukoooo wanawinda na kula wanyama wetu sisi tunatakiwa kutoa macho hata kama ameangukiwa na mti.
 
Pole sana mkuu jifunze kusamehe. Leo kanisani Paroko alitoa mahubiri kuhusu kusamehe. Wakati wa WWII mama mmoja Mjerumani alikuwa mcha Mungu sana alisaidia kuwaficha Wayahudi.

Majeshi ya Hitler yalipata habari hizi, walimvizia na kumkamata. Alipelekwa kwenye torture chamber kwa maagizo kuwa ateswe na daktari kwa lengo ka kuharibu spinal cord ili asiweze kutembea tena.

Daktari alipokuwa anamtesa yule mama alimwambia nimekusamehe kwakua Mungu ni mwema. Kweli yule mama ali paralyse kutokana na mateso lakini alikombolewa.

Miaka takriban kumi baadae daktari alipata ajali na ali paralyse kama yule mama. Alimtafuta yule mama na kumuomba msamaha.
 
Pole sana mkuu jifunze kusamehe
Kuna watu watatu sitamani kuwasamehe katika maisha yangu
mmoja ni huyo tayari ametangulia, mwingine ni mwalimu wa shule ya msingi
alikuwa na ugomvi na mama hasira zake alikuwa anamalizia kwangu shuleni
yule bibi hata kesho namuombea baya limkute wa mwisho ni Polisi ambaye
alinibambikia kesi.
 
Nawe utakufa tu tena sio siku nyingi. Huyo afisa hana kosa, yeye alitekeleza wajibu wake.

5/5
 
Ule ni ubaya mkuu, unawaachaje kanga wajifie na kuoza?

Mkuu sema uliamua kuwa mbinafsi hapo, hata ukiona simba anamla swala, waache ndio nature inavyotutaka na hata hivyo vibudu, kuna wanyama wengine pamoja na wadudu wanategemea ili waweze kuishi, mna bahati hamkupewa kesi ya ujangili
 
Nawe utakufa tu tena sio siku nyingi. Huyo afisa hana kosa, yeye alitekeleza wajibu wake.

5/5
Poa tu ila nashukuru kwa yeye kutangulia maana nilikosa amani kila nikimuona.
 
Kwa uonevu, unyanyasaji na ukandamizaji tunaokutana nao awamu hii natamani kujifunza UCHAWI.
 
Mkuu sema uliamua kuwa mbinafsi hapo, hata ukiona simba anamla swala, waache ndio nature inavyotutaka na hata hivyo vibudu, kuna wanyama wengine pamoja na wadudu wanategemea ili waweze kuishi, mna bahati hamkupewa kesi ya ujangili
Mimi sio miongoni mwa hao wanyama wanaostahili kula wanyama wengine?
 
Back
Top Bottom