Afisa habari wa TFF au Taifa Star?

Afisa habari wa TFF au Taifa Star?

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,709
Reaction score
1,735
WanaJF naomba msinishangae kuuliza swali hili kwani nimejifikiria mno na kutopata jibu. Huyu kaajiriwa na TFF kama afisa habari wake sasa kuongozana na timu ya taifa ambayo tena inaweka kambi nchini Sudan na kujifanya kuwa msemaji wake hii inanitatiza mno. Timu ya taifa ina kocha, msaidizi wake, manager n.k. hao wanatosha kutupa habari ya maendeleo ya timu yetu ikiwa ugenini. Hapa nchini pana mambo mengi tuu yanayotaka ufafanuzi toka TFF ikiwa ni pamoja na Uchaguzi mkuu, sakata la COREFA na ligi (wanayoiita) ya mabigwa inayoendelea nchini, yeye kaongozana na timu kwenda Morocco tena ikiweka kambi Sudan hapa pana ulaji tuu na si kingine.
 
Uko sahihi kabisa mkuu utashangaa timu inasafiri eti na katibu mtendaji anaenda sasa sijui uko shughuli za kitendaji ni zipi si Timu ya Taifa ata Simba na Yanga wana upuuzi huu...Manji alishawahi kumrudishia Airport Katibu Mtendaji timu ilikuwa inaenda kigali Rwanda akamwambia uko wewe unaenda kufanya nini wakati unatakiwa kuendelea na shughuli za kila siku klabuni....bado tunasafari ndefu.
 
Sijui kwa nini hatubadiriki! Hawa wenzetu baba wa taifa aliisha tamka kuwa kule India pakiwa na ujengaji wa daraja basi kazi itaisha tena kwa ufanisi mkubwa na huyo injinia atapata pesa ya ziada ya kukidhi mahitaji yake binafsi, lakini Mtanzania daraja halitoisha ila nyumba yake binafsi itamalizika. Na sisi wadau wa soka tumekaa kimya tu bila kuanzisha mjadala kwenye media kuhusu jambo hili.
 
Mkuu...Kawaida timu ya Taifa inaposafiri huwa kunakuwa na kiongozi kutoka Chama cha Mchezo husika...Sasa huenda Ndg Wambura ndiye aliyepewa jukumu la kusafiri na timu kwenda Morroco kupitia hapo Ethiopia...Kwa mantiki hiyo basi huenda anabeba majukumu yote mawili kwa kuwa kitaaluma nadhani jamaa ni Mwanahabari pia...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom