Afisa Biashara wa Jiji la Arusha asimamishwa kazi na Baraza la Madiwani

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
Habari kutokea Jijini Arusha kwenye Baraza la Madiwani wa jiji hilo zinasema Afisa Biashara amesimamishwa na baraza hilo kutokana na kufanya mchezo mchafu aliyeshirikiana na Diwani wa Moshi Mjini Makoi diwani wa CCM walichezea leseni za jiji hilo kwa kutoa kinamna namna kwenye Maduka ya Makoi

afisa biashara huyo Privanus Katingila amesimamishwa kwa kutoa lesini moja kwenye zaidi ya maduka Ishirini ambayo ni kosa kisheria ambayo niya Makoi Kada Mtifu wa Ccm na Diwani wa Moshi ambaye pia kwenye utawala uliopita wa Madiwani wa Ccm Bwana Makoi amefanya ufisadi Mkubwa kwa kujimilikisha maduka ya Jiji na kuwa mali yake huku Halmashauri ya jiji la Arusha halipati pesa yoyote.

Kioja kingine Bwana Makoi alichofaya baada ya uongozi wa Baraza la Madiwani kumnyanganya maduka ya jiji yeye akafoji barua ya Katibu wa Tamisemi ili aendele kuhodhi maduka hayo lakini Meya na Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kufwatilia ndio wakajua barua hiyo haikutokea kwa katibu wa Tamisemi

hayo ndio kwa ufupi bahadhi ya mambo wana ccm waliopita waliweza kujimilikisha jiji la Arusha kwa Manufa yao binafsi
 
Haki za binadamu watakuja na tamuko la kumtetea kama walivyofanya kwa Kabwe,CDM wataufyata kwa sababu wao ndiyo wanaongoza hilo jiji.
 
Tukifanya mchezo hadi wenye viti wa mitaa nao wataanza kutufukuza wapangaji kisa tumetupa taka mtaani; tangia lini madiwani wakawa na mamlaka ya mwajiri? mpaka wawe na uhalali wa kumfuta mtu kazi.
 
Mkuu Mwanahabari Huru najua unazo taarifa in details, ongezea nyama wadau waelewe jinsi haya manyang'au yalivyoigeuza ofisi ya umma kitoweo
 
Tukifanya mchezo hadi wenye viti wa mitaa nao wataanza kutufukuza wapangaji kisa tumetupa taka mtaani; tangia lini madiwani wakawa na mamlaka ya mwajiri? mpaka wawe na uhalali wa kumfuta mtu kazi.
Usiwe mvivu wa kufikiri, madiwani ni wawakilishi wa wananchi, wananchi wana mamlaka ya kuwawajibisha wahujumu uchumi na mafisadi. Usisahau jana Meya wa Kinondoni alivyomuwajibisha mwanasheria wa manispaa kwa sababu ya kushindwa kutekeleza majukumu yake.
 
Back
Top Bottom