Afisa Ardhi Arumeru Matatani

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amemfukuza kazi Ofisa Ardhi wa Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Nicodemus Hillu, kwa kosa la kurejesha eneo lenye ukubwa wa ekari 3000, kwa mwekezaji Paradeep Lodhia, lililokuwa limefutwa na Rais Dk. John Magufuli.

Katika hatua nyingine, Lukuvi amempandisha cheo aliyekuwa Ofisa Ardhi mteule wa Halmashauri ya Arusha, Rehema Jatto, kuwa Ofisa Ardhi mteule kwenye halmashauri ya jiji la Arusha, baada ya kuridhishwa na utendaji wake wa kazi usio na shaka.

Waziri Lukuvi ameyasema hayo jijini Arusha, wakati akizindua ofisi za ardhi za mkoa wa Arusha na kukabidhi hati za ardhi kwa wananchi zaidi ya 200 waliokuwa wameomba kwa muda mrefu.

Amesema serikali imeamua kurejesha huduma ya ardhi mikoani zikiwa na hadhi ya wizara, ili kuwarahisishia wananchi kupata hati katika maeneo yao na kuwapunguzia gharama za kufuatilia hati maeneo yao ofisi za kanda.

Pia ametoa siku 90 kwa maofisa ardhi nchini, kuhakikisha wanatoa hati za ardhi kwa wananchi ambao wameshapimiwa maeneo yao na kuacha tabia ya kuwazungusha kwa sababu mbalimbali zisizo na tija.
 
Back
Top Bottom