Afghanistan: Bomu lailipuka kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na Rais wa nchi. Watu 24 wauawa

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Watu 24 wamefariki na wengine wengi kujeruhiwa leo, baada ya bomu lililokuwa limetegeshwa kwenye moja ya magari ya Polisi kulipuka Kaskazini mwa nchi hiyo huko Parwan

Hakuna mtu au kikundi chochote kilichojinadi kuhusika na shambulio hilo lililotokea kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliohudhuriwa na Rais wa nchi hiyo, Ashraf Ghani

Msemaji wa Rais katika Kampeni hizo, Hamed Aziz amesema Rais Ghani alikuwepo eneo la tukio lakini yupo salama na wala hajajeruhiwa, na taarifa zaidi atatoa baadaye

Aidha, Msemaji wa Gavana wa Parwan, Wahida Shahkar amesema shambulio hilo limetokea katika eneo la kuingilia ukumbini, wakati mkutano ukiendela
******

Afghan officials say a sticky bomb attached to a police vehicle went off near a campaign rally by President Ashraf Ghani in the country’s northern Parwan province.

At least 24 people were killed and dozens more wounded after an IED attached to a security vehicle exploded near a campaign rally attended by Afghan President Ashraf Ghani, potentially marking an attempt on his life

The president’s campaign spokesman Hamed Aziz says that Ghani was there but that he is safe and unharmed. Aziz said he would provide more details later.

Wahida Shahkar, spokeswoman for the provincial governor in Parwan, says the explosion happened while the rally was underway on Tuesday, at the entrance to the venue.

No group immediately claimed responsibility for the attack.
 
Sio habari ngeni huko Afaghastan.Mabomu huko kama singeli Dar
 
Lilitegwa kwenye gari ya police? Hiyuo nchi hao maharamia wana intelligence kali sana
 
Back
Top Bottom