singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeipongeza Tanzania baada ya Uganda kuamua hivi karibuni kuwa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda litapita katika ardhi ya Tanzania hadi bandari ya Tanga.
Pongezi hizo zimetolewa na Mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo, Tonia Kandiero wakati alipofika katika Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam na kuzungumza na uongozi wa wizara ukiongozwa na Waziri Profesa Sospeter Muhongo pamoja na watendaji wa taasisi zilizo chini ya wizara.
“Tunawapongeza sana kwa kupata mradi huu muhimu kwa nchi ya Tanzania, napenda kukutaarifu kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika ipo tayari kufanya kazi nanyi ili mradi huo uweze kutekelezeka kama ilivyopangwa,” alisema Kandiero.
Akizungumzia utekelezaji wa bomba hilo litakalokuwa na urefu wa kilometa 1,403 na kipenyo cha inchi 24, Profesa Muhongo alisema hatua inayofanyika sasa ni majadiliano ya wataalamu kutoka nchi hizo mbili juu ya mpango wa utekelezaji wa mradi huo, ikiwemo masuala ya fedha na watatoa taarifa yao kwa viongozi wa juu wa nchi hizo.
Alisema pia kitajengwa kiwanda kwa ajili ya kusafisha mafuta ghafi katika eneo la Hoima, na mradi huo utagharimu Dola za Marekani bilioni 4.7 na kila nchi mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki atakuwa na hisa ya asilimia nane na kuwajibika kuchangia Dola za Marekani milioni 150.4 ili kutekeleza mradi huo.
“Sisi kama nchi tunajipanga kuchukua asilimia zote nane za hisa hizo na fedha ambazo tunapaswa kutoa kwenye mradi huu zinaweza kutoka serikalini au sekta binafsi hivyo tunaweza kuja AfDB kuzungumza suala hili,” Profesa Muhongo alimueleza Mwakilishi Mkazi huyo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika.
Aidha, AfDB iliipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kutekeleza mikakati mbalimbali inayowezesha deni la shirika kupungua.