Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,865
- 3,802
Nimefatilia vizuri mashindano ya AFCON yanayoendelea kule Ivory cost, nikagundua kama huna wachezaji ambao wako fiti kwa maana ya nguvu, utimamu wa mwili,wenye maumbo makubwa na waonajituma ni ngumu kushinda mechi. Lazima uwe na wachezaji ambao wako fiti kweli kweli na wenye "spirit" ya kulazimisha mambo yatokee bila kujali zimebaki dk ngapi. Ndio maana tumeshuhudia matokeo ya kushangaza.
Timu yetu inawacheza wengi ambao hawawezi kupambania "dual balls".Pia wengi ni wafupi na hawana utimamu wa mwili wa kutosha kumudu kucheza dk 90 zenye mbilinge mbilinge. Fikiria unamtoa Kibu Denis halafu unamuingiza Charles Mmombwa, halafu mechi imechafuka Zambia wanalitaka goli wapi na wapi!!. Kwenye timu yetu tuna wachezaji wachache sana wenye nguvu na spirit ya kupambana mfano Kibu Denis, Ibrahimu Baka, Mzamiru, Novatus na Himidi Mao. Wengine na wazuri tukiwa na mpira basi "the likes of Feitoto"
Wapo wachezaji ambao huwa tunawachukulia poa lakini kwenye haya mashindano ya mechi 3 muhimu wangeweza kutusaidia. Mfano Laurent Lusajo, Tariq Seif, Masawe( japo umri umeenda), Charles Ilafya na Kelvin Kijili. Hawa ni baadhi ya wachezaji wachache tulionao ambao wana maumbo na makubwa na roho ya upambanaji, japo wanaweza wasiwe wazuri wa kuuchezea mpira. Ndio Ditramu Chimbi katika ubora wake aliwahi kuwa mchezaji muhimu sana kwenye timu yetu.
Kutokana kukosa wachezaji wa aina hii ndio maana inakuwa vigumu Taifa Stars kufunga magoli ya kona au faulo ila ni rahisi sana sisi kufungwa magoli ya aina hiyo. Ni kweli wenzetu wametuacha ila tumeshuhudia timu za viwango vyetu zikifanya maajabu ya kuwapiga vigogo kutokana na kutumia wachezaji wenye hizo sifa nilizozieleza. Nadhani somo limetuingia. Next time viongozi na benchi la ufundi wawe makini kwenye "selection" ya wachezaji. Kwenye timu ya Taifa ufundi na kipaji cha kuuchezea mpira havitoshi kupata matokeo. Ni zaidi ya hivyo. Nawasilisha.
Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app