AFCON 2015: Nigeria na Uganda nje, Tembo wanusurika

AFCON 2015: Nigeria na Uganda nje, Tembo wanusurika

Lupweko

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
25,195
Reaction score
27,377
Mabingwa watetezi wa Kombe la Mataifa ya Afrika, timu ya taifa ya Nigeria, imekosa tiketi ya kushiriki fainali za kombe hilo kwa mwaka 2015 nchini Guinea ya Ikweta baada ya kutoka sare nyumbani ya mabao 2-2 na timu ya taifa ya Afrika ya Kusini, Bafana Bafana. Nigeria imejikuta ikishika nafasi ya tatu katika kundi A nyuma ya South Africa na Congo. Wakati huo huo, katika kundi F, majirani zetu Uganda nao wamekosa nafasi hiyo baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 ugenini mbele ya Guinea. Uganda ilihitaji sare ya aina yoyote kufuzu.

Katika michezo mingine ya makundi tofauti, Ivory Coast nayo imenusurika kuzikosa fainali hizo baada ya kutoka sare nyumbani ya 0-0 na Cameroun. Congo DRC ilikuwa inavizia Ivory Coast iteleze ili ifuzu. Zambia imejitutumua na kuichapa timu ngumu ya Cape Verde kwa bao 1-0
 
Kwani hakuna sheria ya bingwa mtetezi kushiriki moja kwa moja kama ilivyo kwa muaandaaji!!?.
 
Uganda wamekosa tena....dah...
uganda niwa hapahapa acha tu waendelee kutuongozea kwenye ranking za fifa kuhusu kufuzu afcon mpaka sisi tufuzu ikibidi wote east afrika kenya uganda na tanzania vinginevyo acha tuendelee kuwashangilia waliozoea kwenda
 
Back
Top Bottom