AfCHPR yaitaka serikali ya Tanzania kutotekeleza hukumu ya kunyongwa hadi kufa dhidi ya Amini Juma

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,005
5,550
Serikali ya Tanzania imetakiwa kutotekeleza hukumu ya kunyongwa hadi kifo iliyotolewa na Mahakama ya Rufaa dhidi ya ndugu Amini Juma. Ombi hilo limetolewa na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu (AfCHPR). Mahakama hiyo imetoa ombi la kutotekelezwa kwa hukumu hiyo hadi pale maombi aliyoyawasilisha bwana Amini Juma yatakapotolewa ufafanuzi.

Aidha Mahakama hiyo pia imeitaka Serikali kutoa taarifa za utekelezaji wa maagizo yake ndani ya siku 60 baada ya kupokea taarifa rasmi za AfCHPR. Bwana Amini Juma anadai kuwa baada ya hukumu ya Mahakama ya Rufaa alitoa maombi ya kupitiwa upya hukumu yake, lakini Mahakama imechelewesha kufanya hivyo hadi alipowasilisha maombi yake AfCHPR Aprili katika kesi iliyopewa namba 024/2016.

Hukumu hiyo ilitolewa kwa bwana Amini Juma baada ya kukutwa na hatia ya kutekeleza mauaji ya Meserani huko Monduli mkoani Arusha mnamo Septemba 18, 2008. Sasa mhukumiwa anashikiliwa katika gereza la Maweni mkoani Tanga. Amini Juma alikata rufaa kupinga hukumu hiyo lakini Mahakama ya Rufaa iliitupilia mbali hukumu hiyo na kuamuru mtuhumiwa anyongwe hadi kifo.
 
Wasiwe na wasiwasi hakuna Raisi wa Tanzania mwenye ujasiri wa kusaini hukumu ya kifo
 
Back
Top Bottom