AFC Leopards vs Yanga

The Sun-of-a Beach

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
1,245
2,000
Ni dakika ya 51:03' hadi sasa, na matokeo ni 0 - 0.
Naona Yanga wanajitahidi ku-perform hapa, wamewazidi kiasi AFC (moja ya timu kubwa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki). Yanga wameonyesha ku-improve kwenye mechi hii, tofauti na ile waliyocheza dhidi ya Polisi waliyolala 2 - 0. Pamoja na hayo, hii mechi haivutii kabisa na baada ya dakika chache naona ni heri nikacheze draft barazani kuliko kuona huu upuuzi unaoendelea hapa.
Nimegundua kwamba, ukitoka kuangalia mechi ya Simba ndani ya saa 24 au siku 3, hutakiwi uangalie mechi yoyote ya Yanga, maana lazima utakereka tu.

Dakika ya 63' anatoka Sadney, anaingia Mrisho Ngasa.Ngasa anashangiliwa kweli kweli (hii ni dalili nyingine ya kupoteana,Ngasa anashangiliwa?)

Dakika ya 71' Jaffar Owiti wa AFC, aliyewakosa kosa Yanga hivi punde, anatolewa.

Namwona Molinga "jumba kubwa" anapasha misuli nje ya uwanja.
Huyu jamaa ni mzito kama gari la mkaa, na ni mzigo kama gunia la mbolea ya Urea.Kuna la maana atafanya leo huyu?

Dakika ya 75:36' Vincent Akamahoro wa AFC anatolewa.Na Yanga wanakoswa koswa.

Dakika ya 77:39' Sibomana anakosa bao, baada ya kumegewa pande zuri kutoka kwa uncle Mrisho Ngasa.

Dakika ya 77:52' AFC wanapata kona na lahaulaaaaa wanakosa bao!

Dakika ya 83' Yanga wanapata kona.Na Goooooaaaaal...Papy Kabamba Tshishimbi anapiga kichwa na kuukwamisha mpira wavuni. AFC 0 - 1 Yanga.

Dakika ya 87:35' Issa Bigirimana anaingia kuchukua nafasi ya Patrick Sibomana kwa upande wa Yanga. Huyu Sibomana ndiye aliyepiga kona iliyozaa goli ya Yanga.

Dakika ya 90:04' Vicent Oburu wa AFC anakula umeme (red card) kwa kumfanyia madhambi Tshishimbi.

Dakika ya 93' AFC wanapata faulo.Ni eneo zuri kwa wapigaji wazuri.Yanga na AFC wanabishana kuhusu kuweka ukuta.
Faulo ya hovyo inapigwa na AFC wanakosa nafasi ya pekee.

Dakika ya 95:35' Mpiraaaaa umekwishaaaaaa..AFC 0 - 1 Yanga.

Hongereni watani zetu Kwasukwasu, Mbutembute FC kwa ushindi huu.Ila mnapaswa kuongeza bidii zaidi.Mna kazi nzito huko muendako.

Namwona 'msemaji' wa Yanga, yule anavaa kofia kama Profesa Ndumilakuwili (Mwinyi Zahera) anajisogeza kwenda kuhojiwa. Na mimi sisikilizagi upupu!

Jioni njema.
 
Sobangeja

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
354
500
Ni dakika ya 51:03' hadi sasa, na matokeo ni 0 - 0.

Naona Yanga wanajitahidi ku-perform hapa, wamewazidi kiasi AFC (moja ya timu kubwa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki). Yanga wameonyesha ku-improve kwenye mechi hii, tofauti na ile waliyocheza dhidi ya Polisi waliyolala 2 - 0.

Pamoja na hayo, hii mechi haivutii kabisa na baada ya dakika chache naona ni heri nikacheze draft barazani kuliko kuona huu upuuzi unaoendelea hapa.

Nimegundua kwamba, ukitoka kuangalia mechi ya Simba ndani ya saa 24 au siku 3, hutakiwi uangalie mechi yoyote ya Yanga, maana lazima utakereka tu.
Acha uongo,hiyo Ni Arusha Football Club.
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
10,249
2,000
Hii ndiyo Yanga ya wananchi! Kwa upangaji huu wa timu, hata ikatokea tukafungwa nitakubali matokeo. Siyo ile Yanga ya akina Ali Ali iliyocheza na Polisi.
 
ZionGate

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
5,803
2,000
Ni dakika ya 51:03' hadi sasa, na matokeo ni 0 - 0.

Naona Yanga wanajitahidi ku-perform hapa, wamewazidi kiasi AFC (moja ya timu kubwa kwenye ukanda wa Afrika Mashariki). Yanga wameonyesha ku-improve kwenye mechi hii, tofauti na ile waliyocheza dhidi ya Polisi waliyolala 2 - 0.

Pamoja na hayo, hii mechi haivutii kabisa na baada ya dakika chache naona ni heri nikacheze draft barazani kuliko kuona huu upuuzi unaoendelea hapa.

Nimegundua kwamba, ukitoka kuangalia mechi ya Simba ndani ya saa 24 au siku 3, hutakiwi uangalie mechi yoyote ya Yanga, maana lazima utakereka tu.
Ni sawa na kunywa balimi alafu ukachanganye na mataputapu..
 
ZionGate

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
5,803
2,000
Wachezaji wa Yanga wanarukaruka tu hapa, wamekoswakoswa hapa mpira umegonga mwamba,.
Yangwa level yake waimba kwaya au bodaboda...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom