Afariki dunia mara baada ya kupigwa na fimbo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afariki dunia mara baada ya kupigwa na fimbo

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Gumzo, Jul 14, 2012.

 1. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  MKAZI mmoja wa kijiji cha Piyaya kilichopo wilayani Ngorongoro aliyefahamika kwa jina la Alaisieleke Korio (48) amefariki dunia baada ya kupigwa fimbo kichwani na mwenzake .


  Kamanda wa polisi mkoani hapa, ACP Liberatus Sabas alisema kuwa marehemu huyo alipigwa fimbo kichwani na mtu aliyefahamika kwa jina la Zablon Shilalo(32) mkazi wa Ingarasero wilayani Ngorongoro.


  Alisema kuwa, tukio hilo limetokea july 8 mwaka huu majira ya saa 7;00 usiku katika kijiji cha Piyaya kilichopo wilayani Ngorongoro mkaoani Arusha.


  Sabas alisema kuwa ,chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi uliotokana na madai ya fedha kati ya marehemu mtuhumiwa ambapo marehemu alikuwa anakumbusha deni lake kwa mtuhumiwa huyo , hali iliyozusha mabishano kati yao wawili.


  Alisema kuwa,kutokana na mabishano hayo ndipo mtuhumiwa alichukua fimbo na kumpiga marehemu aliyepata jeraha kichwani ambalo lilimsababishia kifo chake.


  Aidha Kamanda Sabas aliongeza kuwa, kufuatia tukio hilo jeshi la polisi mkoani hapa linaendelea na uchunguzi zaidi wa kumhoji mtuhumiwa huyo kutokana na tukio hilo.

  Alisema kuwa,mara baada ya uchunguzi huo ,mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kujibu shitaka hilo la mauaji hayo na mwili wa marehemu umeshazikwa baada ya kufanyiwa uchunguzi na daktari wa hospitali ya Wasso.

  Wakati huo huo, mtoto wa siku moja wa jinsi ya kiume amekutwa akiwa ametupwa katika eneo la Mianzini mjini hapa .

  Aidha mtoto huo alikutwa akiwa amefunikwa kwenye mfuko wa rambo ambapo kugundulika kwa mtoto huyo ni baada ya mbwa aliyekuwa akila jalalani kuona mfuko huo na kuanza kuufungua akidhani ni chakula. KWA HABARI KAMILI BOFYA HAPA
  GUMZO LA JIJI: AFARIKI DUNIA MARA BAADA YA KUPIGWA NA FIMBO
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Duh! Ama kweli ukishamwaga damu ya mtu hakika hauendi mahala!

  R I P marehemu A. Korio!

  Na huyu naye aliyetupata mtoto angetakiwa akamatwe na kesi yake iendeshwe sawa na huyu mhalifu tajwa hapo juu!
   
Loading...