Afariki dunia baada ya kuzama baharini

Afariki dunia baada ya kuzama baharini

Ryan Herman

Member
Joined
Jul 26, 2019
Posts
42
Reaction score
46
Haji Ali Haji mwenye umri wa miaka 55 Mkaazi wa Jambiani Mfumbwi amefariki dunia baada ya kuzama bahari wakati akiwa katika shughuli zake za uvuvi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Suleiman Hassan Suleiman amesema tukio hilo limetokea majira ya saa kumi na dakika ishirini jioni katika bahari ya Jambian Mfumbwi na mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi katika Hospital ya Cottage Makunduchi na kukabidhiwa kwa jamaa zake kwa ajili ya mazishi .

Hata hivyo Sheha wa Shehia ya Jambiani Kikadini Hassan Haji Maringo amekiri kutokea kwa tukio hilo la kuzama bahari kwa mtu huyo ambae ni mvuvi mahiri sana na kuwataka wavuvi wasipendelee kuenda baharini pekee yao na baadala yake wafatane ili panapotokea tatizo wasaidiane.

Sambamba na hayo Kamanda Suleiman ametoa wito kwa jamii na wananchi wote waliopo katika mkoa huo kuwa na mashirikiano pindi pale wanapokwenda katika uvuvi wa baharini kwani wanapokuwa na mashirikiano wanaweza kusaidiana panapotokea tatizo.
 
Back
Top Bottom