Afariki dunia baada ya kutumbukia katika shimo la choo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afariki dunia baada ya kutumbukia katika shimo la choo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 11, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  IJANA Maneno Juma amefariki dunia baada ya kutumbukia kweye shimo la choo wakati akiwa katika harakati za kutengeneza choo hicho huko maeneo ya Ilala Bungoni jijini Dar es Salaam..
  Marehemu Maneno alifika katika nyumba hiyo akiwa na vijana wenzake wengine wawili baada ya kupewa tenda ya kurekebisha choo hicho.

  Hivyo imedaiwa kuwa wakati wakiwa katika harakati za utengenezaji wa choo hicho kwa bahati mbaya alitereza na kutumbukia katika shimo la choo hicho ambalo lilidaiwa lilikuwa limejaa kinyesi na maji.

  Kwa kuwa shimo hilo lilikuwa limejaa maji hayo machafu na kinyesi hicho marehemu alipoteza maisha kwa kushindwa kujiokoa mwenyewe na juhudi za kuupata mwili huo zilifanyika mara baada ya kufika kwa waokoaji kutoka Halmashauri ya Jiji.

  Waokoaji hao walinyonya maji taka na kinyesi toka kwenye shimo la choo la hicho ambapo walifanikiwa kuupata mwili wake.

  Tukio hilo lilisikitisha watu wengi waliofika eneo hilo na baada ya kuona mwili huo ukitolewa shimoni humo huku ukiwa umetapatakaa kinyesi.

  Watu wengi walikuwa wakimwaga machozi kwa kijana huyo kupoteza maisha yake akiwa katika harakati za kuisaka shilingi.

  Mwili huo ulichukuliwa na kwenda kuhifadhiwa hospitali ya Amana.
  Tukio hilo lilitokea jana.
   
Loading...