Afanya Maombi Kuliondoa 'Pepo' la Mwenye Nyumba Wake

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
IKIWA hiii ni wiki ya mwisho kodi ya pango ya nyumba alilolipia inamalizika, mwanamke aliyeripotiwa katika mtandao huu kuwa anasababisha kelele kwa wapangaji wenzake, inadaiwa anazidisha maombi kumuombea mwenye nyumba ili aweze kurudisha moyo wake.
Chanzo cha habari hii kinadai kuwa, mwanamke huyo alipewa notisi na mwenye nyumba kutokana na kusababisha kadhia kwa wapangaji wenzake kwa kufanya maombi kwa sauti ya juu chumbani kwake na kusababisha kelele na kupoteza amani kwa wapangaji wenzie ndani ya nyumba hiyo.

Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo awali alionywa na mmiliki wa nyumba hiyo aliyetambulika kwa jina moja la Mzee Hussein kuwa asiwasumbue wapangaji wenzake na alimsihi mpangaji wake huyo kuendesha maombi chumbani kwake bila kusababisha usumbufu kwa wenzake.

Imedaiwa kuwa mwanamke huyo alikiuka maagizo hayo na aliamua kuleta waumini wenzake chumbani na kufanya maombi kwa sauti ya juu kwa masaa mawili ama matatu mfululizo na kusababisha upotevu wa amani kwa wapangaji wengine.

Hivyo kutokana na kadhia hiyo kupinduka mipaka wapangaji wengine waliripoti kadhia hiyo kwa mmiliki wa nyumba hiyo na mwanamke huyo kutakiwa kuhama kwenye nyumba kutokana na kero hiyo.

Hata hivyo ilidaiwa mwanamke huyo alimuomba mwenye nyumba huyo asimpe notisi kwani ataacha kufanya maombi kwa sauti kubwa lakini hali hiyo ilipozidi kuendelea mwenyewe nyumba aliamua kumpa notisi mwanamke huyo.

Hivyo imedaiwa mwanamke huyo mwishoni mwa juma lililopita alianzisha maombi na waumini wenzake kwaajili ya kumuombea mmiliki huyo aondokane na pepo lilipompata la kuchukua uamuzi wa kumfukuza toka kwenye nyumba hiyo.

Imedaiwa maombi hayo juzi, jana yalifanywa kwa takribani masaa mawili akishirikiana na waumini wenzake kulitoa pepo lililompata mwenye nyumba hiyo.

Juhudi za Nifahamishe.com za kutaka kuwasilina na mwenye nyumba kujua kama "pepo" lake la kumfukuza mwanamke huyo limetoka au la hazikuzaa matunda kwa kuwa namba yake ya simu ya mkononi ilikuwa haipatikani.
 
Back
Top Bottom