Afande Sele: MO Dewji ni mpiga dili hana nia ya kuwekeza kweli kwenye soka

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,250
15,116
Hizi stori za kununua mchezi mbona kama zina mashiko. Maana mabao ya Penati yalikuwa mengi sana msimu huu.

Hizi stori za kununua marefa mbona zimekuwa nyingi. Maana mabao ya offside yalikuwa mengi sana msimu huu, mpaka pale mashabiki wa Yanga walipopaza sauti mitandaoni.

Lakini pia huenda wakawa wabovu kupindukia, mbona wameshindwa kupata matokeo mazuri na timu ambazo hazinunuliki kwa pesa ya Madafu.

Young Africans1-0Simba SC
Simba SC0-1JKT Tanzania
Simba SC2-2Young Africans
Simba SC0-0Tanzania Prisons
Mwadui1-0Simba SC
Mtibwa Sugar0-0Simba SC
Simba SC1-1Biashara Mara United

(zingatia aina ya timu ambazo wameshindwa kupata matokeo)

Je pia ni kweli kusema ndio timu pekee yenye wachezaji wenye wastani mkubwa wa umri.

Afande sele alitupatia Jawabu Mubashara. (SHABIKI NAMBARI ONE WA SIMBA)

Ukweli ni kwamba timu yetu Simba huwa inashinda mechi nyingi kwa kununua timu pinzani au marefa lakini ni mbovu sana imejaa wachezaji wazee na magarasa ndio maana mimi namuona hata MO Dewji ni mpiga dili hana nia ya kuwekeza kweli kwenye soka'' Afande Sele, shabiki mkubwa wa Simba
 
"Akili ni nywele" nadhani jamaa alipokosa akili akaamua kufuga nywele ili ajifariji kuwa ana akili ila akaambulia patupu.

Huyu jamaa heshima yake inashuka kila siku kama theluji ya mlima Kilimanjaro.
 
Hizi stori za kununua mchezi mbona kama zina mashiko. Maana mabao ya Penati yalikuwa mengi sana msimu huu.

Hizi stori za kununua marefa mbona zimekuwa nyingi. Maana mabao ya offside yalikuwa mengi sana msimu huu, mpaka pale mashabiki wa Yanga walipopaza sauti mitandaoni.

Lakini pia huenda wakawa wabovu kupindukia, mbona wameshindwa kupata matokeo mazuri na timu ambazo hazinunuliki kwa pesa ya Madafu.
Young Africans1-0Simba SC
Simba SC0-1JKT Tanzania
Simba SC2-2Young Africans
Simba SC0-0Tanzania Prisons
Mwadui1-0Simba SC
Mtibwa Sugar0-0Simba SC
Simba SC1-1Biashara Mara United

(zingatia aina ya timu ambazo wameshindwa kupata matokeo)

Je pia ni kweli kusema ndio timu pekee yenye wachezaji wenye wastani mkubwa wa umri.

Afande sele alitupatia Jawabu Mubashara. (SHABIKI NAMBARI ONE WA SIMBA)

View attachment 1382063
Hujui unachokiongea wewe. Mtibwa kafungwa michezo yote miwili aliyokutana na Simba.
Biashara naye kafungwa michezo yote aliyokutana na Mnyama.

Jifunze kuheshimu matokeo ya timu pinzani. Tunatamani tushinde kila mchezo, mpira unakuwa mtamu zaidi kukiwa na matokeo kama haya ili yaweze kutujenga zaidi na zaidi
 
Kwa lipi Biashara United isinunulike ilhali kila siku RC Malima anatembeza harambee kuikwamua na ukata?

Yaani Azam inunulike halafu Biashara ipone!
 
Kwa lipi Biashara United isinunulike ilhali kila siku RC Malima anatembeza harambee kuikwamua na ukata?

Yaani Azam inunulike halafu Biashara ipone!
Nina uhakika wakati anayazungumza/kuandika hayo alikuwa kavuta bange
 
Thread Ya Ajabu Sana Hii
Sasa Anayeamua Kaamua Vingine Lawama Ndiyo Zinaenda Kwa Simba. Goal Ikaamuliwa Kona Utalaumu Nini, Refa Kwa Maamuzi Ama Wananunua.
 
Hiyo afande wenu hajielewi, sasa kama Simba akishinda game zake amenunua, na kama Simba aliweza kuifunga Azam kwa kununua matokeo, kwanini Simba ishindwe kuwanunua Mwadui?!

Yupi mwenye bei kubwa kati ya Azam na Mwadui kwa mujibu wa mtazamo wa huyo afande?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu na hii ndio shida ya kuvuta bange kabla hujatia chochote tumboni..
 
mabangi yanamsumbua. mimi najiuliza kwani Mo ndo anaecheza au kuna wachezaji wanadai mishahara hawajalipwa?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom