Mo Dewji na safari ya kuwa Mwanahisa halisi wa simba sports club

Mnyuke Jr

JF-Expert Member
Jul 3, 2021
4,471
6,371
Simba sports club ni moja kati ya timu za ligi kuu Tanzania bara ambayo imekuwa ikiendelea na mchakato wa kufanya mabadiliko ya uendeshaji wa timu.

Mwekezaji Mo Dewji ambaye ni shabiki na mwanachama wa timu hiyo aliyeamua kununua 49% ya hisa za klabu ili mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji uweze kukamilika huku wanachama wakibaki na hisa 51% ambazo zinawafanya kuwa na nguvu katika maamuzi ndani ya timu hiyo.

Kufuatia mchakato huo na uwekezaji alipofanya ndani ya timu kwa sasa anataka kubaki kama mwekezaji tu na kujiweka mbali na shughuli nyingi za timu hiyo kwa kuanza tu ameanza na vitu vifuatavyo:-

1. Kujiuzulu nafasi Uenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa simba Sports Club na kumuachia nafasi hiyo Salim Abdallah "Try Again", na lengo lake ni kubaki mwekezaji tu wa timu hiyo.

2. Muwekezaji wa klabu ya Simba SC Mohammed Dewji amewa - UNFOLLOW wachezaji wote wa klabu ya Simba SC pamoja na wafanyakazi wa klabu hiyo, pia akibakisha Account ya Simba wa wanaume na wanawake

- Amebakiza majina (40) pekee ya watu aliowafollow, majina mengi kati ya hayo 40 ni watu binafsi na makampuni.

Baada ya Rais wa Heshima Simba, Mohammed Dewji ku-unfollow wachezaji wa timu hiyo katika akaunti yake ya Instagram sasa ame unfollow na klabu hiyo akibakisha ya Simba Queens ambayo aliipongeza kwa ushindi wao juzi wa mabao 7-0 dhidi ya JKT Queens.

Pia aliweza kuacha kutoa Bonus zote kwa wachezaji ikitokea wamefanya vizuri katika michezo kwa lengo la kuboost morali za wachezaji wa timu hiyo.

Amefanya yote hayo kwa lengo la kupunguza lawama anazopewa kila siku na mashabiki wa timu hiyo ikitokea timu yao imefanya vibaya uwanjani na anafanya hivyo kwa lengo la kujiweka sawa na wawekezaji wenzake kutoka Yanga ambaye ni Gharibu Said Mohammed na Azam ambaye ni Said Salum Bakhresa ambao wapo nyuma ya uendeshaji wa timu hizo bila kuonesha makucha yao.

Ni jambo la muhimu sana kwake kujiweka mbali na uendeshaji wa timu hiyo wa kila siku kwa afya ya kampuni zake za METL ambazo ndio msingi wa utajiri wake mkubwa hapa nchini

Kila lenye kheri Mo Dewji katika uwekezaji wako madhubuti kwa timu uipendayo zaidi duniani
 
Mo siyo mdhamini, ni mwana hisa (mmiliki wa Simba sc kwa 49% )
Kwani mchakato umekamilika?

Hili ni swali ambalo mwekezaji huyo aliuliza mjini twitter na kuna uwezekano hata hiyo Bilion 20 akaitoa kwa sababu kuna uwezekano hata huo mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo haujakamilika
 
Kwahivyo ulitaka MO azaliwe Scotland ndo aje kuwekeza Simba SC..Hivi mtaacha lini kubeza vya kwenu, haya wewe shabiki la Yanga umezaliwa wapi?

Acheni utumwa wa mawazo nyie..!
Punguza jazba
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom