Asante sana kwa maoni yenu, nimeyapokea. Napenda kutoa majibu/maoni kama ifuatavyo;
1. Demo si kwa ajili ya kuuza, ila kuna kampuni inaihitaji ili kama concept itakubalika iweze kupata ufadhili na vipindi viweze kunadaliwa ili kuleta mapinduzi ktk tasnia ya suala zima la kumkuza mtanzania ktk 'career' fulani na suala zima la utafutaji kazi/kujiajiri.
2. Hakika ni kujitolea kwa sababu demo yenyewe haina malipo yoyote. Lakini pia ni vizuri kuweka sense ya volunteerism/kujitolea. Kila jambo unaloshiriki kuna faida ya ku-expose skilla zako, na pia ni rahisi kwa kampuni kukutumia baadae ktk mambo mengine ambayo wewe utalipwa. Kwa mfano tu, mimi kama nina muda na sehemu kama kuna semina, nitahudhuria hata kama watasema niwaandikie report, najua kwa kuwa ni seminar vitu vingi nitajifunza
3. Nimesema mafunzo tutatoa bure kabla ya kuandaa hiyo demo, hayo mafunzo ni fursa kwa mshiriki kujinoa zaidi ktk mambo yake.
Natanguliza shukrani