Adui wa maslahi ya mfanyakazi ni mfanyakazi mwenyewe.

wazunguwawili

JF-Expert Member
May 29, 2019
3,984
4,131
Salam za mei mosi ndugu watanzania.

Salam za idd el fitri ndugu wananchi.

Nipo hapa natazama TBC maadhimisho ya mei mosi 2022 huku nikipitia baadhi ya nyuzi za wadau humu.

Ukitazama kila changamoto inayowakumba wafanyakazi chanzo ni wao wenyewe.

Mfano kuhusu kikokotoo, mafao ya kujitoa ni wafanyakazi waliokasimiwa mamlaka ndiyo wanawatesa wafanyakazi wengine.

Ukija upande wa kodi, hapa nazungumzia PAYE. Niwafanyakazi wanaohusika kuweka mikakati.

Hata hawa wanasiasa walishakuwa wafanyakazi na wanaelewa madhira yote yanayowakuta wafanyakazi.

Wafanyakazi ndiyo wataalam,waweka mipango,watelezaji wa sera na karibu kila kitu kuendelea kwa hii nchi mchango wao ni mkubwa.

Wanapokuwa wanalalamika tu kana kwamba kuna kundi lingine huwa nawashangaa sana.

Wamekuwa watu wa kudai dai tu. Kuonewa onewa tu.

Nawashauri wafanyakazi kila mtu kwa nafasi yake muda wote wajitazame wao katika kulinda maslahi yao wenyewe.

Vinginevyo mtangoja kila mei mosi.
 
Back
Top Bottom