Uzuri ni kwamba EZOIC wenyewe wana feature inaitwa MEDIATION, hii inakuwezesha kuonesha matangazo ya Adsense na EZOIC kwa wakati mmoja na kupata hela kwa wakati mmoja. Hela za ADSENSE zitaenda kwenye account yako ya ADSENSE na hela za EZOIC zitabaki EZOIC.
Kwa Mediavine na Adthrive wao hio feature ya MEDIATION hawana, ila kwa sababu ni GOOGLE CERTIFIED PARTNERS utapata matangazo yote ya Adsense ila ni yale yenye thamani kubwa tu kupitia Google Double click program. Hivyo hutahitaji haya matangazo 'uchwara: ya Adsense.
Factors ni nyingi sana ila kubwa ni seasonality ( msimu) kama vile bei za mazao zinavhopanda na kushuka.
Kwa msimu wa quarter ya tatu (july-sept) Maadvertiser (makampuni) wengi hawako tayari kutumia hela nyingi kwenye online ads kutokana na hali ya biashara zao kwa kipindi hiki, hivyo kupelekea competition kupungua, competition ikipungua automatically bidding price inapungua na ndo CPC na CPM zinashuka.