Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, amesema kukosekana kwa Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi kumeendelea kuwa chanzo cha wananchi wengi “kulia machozi ndani ya mioyo yao,” akiahidi kupigania mabadiliko hayo ndani ya Bunge bila kuchoka.
Ado alitoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Baraza la Idd, Tunduru Mjini, akiwa katika ziara yake ya kuwashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa kumchagua kuwa mbunge.
“Na hali hiyo inatokea kwa sababu Tanzania hatuna Katiba Mpya na hatuna Tume huru ya uchaguzi. Na mimi nawaambia, sitolala; nitambana Spika Zungu ndani ya Bunge mpaka Tanzania ipate Katiba Mpya ili kwenye uchaguzi anayeshinda ashinde na anayeshindwa ashindwe.
Lakini pia nilimwambia Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ahakikishe rasilimali za wananchi zinatumika kwa ajili ya maendeleo ya wananchi, sio mafisadi wachache,” amesema Ado.
Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, amesema kukosekana kwa Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi kumeendelea kuwa chanzo cha wananchi wengi “kulia machozi ndani ya mioyo yao,” akiahidi kupigania mabadiliko hayo ndani ya Bunge bila kuchoka.
Your browser is not able to display this video.
Ado alitoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Baraza la Idd, Tunduru Mjini, akiwa katika ziara yake ya kuwashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa kumchagua kuwa mbunge.“Na hali hiyo inatokea kwa sababu Tanzania hatuna Katiba Mpya na hatuna Tume huru ya uchaguzi.
Na mimi nawaambia, sitolala; nitambana Spika Zungu ndani ya Bunge mpaka Tanzania ipate Katiba Mpya ili kwenye uchaguzi anayeshinda ashinde na anayeshindwa ashindwe.Lakini pia nilimwambia Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ahakikishe rasilimali za wananchi zinatumika kwa ajili ya maendeleo ya wananchi, sio mafisadi wachache,” amesema Ado.