Ado Shaibu awashukuru Tunduru Kaskazini

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
609
1,540
ADO SHAIBU AWASHUKURU TUNDURU KASKAZINI.

Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ndugu Ado Shaibu ambaye alikuwa Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini Kwenye Uchaguzi Mkuu 2020 amefanya ziara Katika Kata ya Muhuwesi.

Kwenye Kikao cha ndani Cha Wanachama, Ndugu Ado ameshukuru Wanachama wa Kata ya Muhuwesi kwa sababu kwenye Uchaguzi wa Mwaka 2020, licha ya kutawaliwa na hujuma kubwa, wagombea wa ACT Wazalendo walishinda kwenye vijiji vya Muhuwesi na Msagula.

Ndugu Ado amewaeleza wanachama hao kuwa yeye anaamini kuwa Uongozi ni wito hivyo licha ya kutotangazwa mshindi, ataendelea kuwapigania Wananchi wa Muhuwesi na Tunduru kwa ujumla kwenye kero mbalimbali zinazowakabili.

"Wale waliodhani watatukatisha tamaa kwa kutuhujumu kwenye Uchaguzi wamepoteza muda wao. Mimi najihesabu kuwa ni Mbunge Nje ya Bunge. Nitapaza sauti dhidi ya madhila mbalimbali yanayowakuta Wana Tunduru".

Ndugu Ado amewaahidi vijana wa Muhuwesi kuwa atakuwa Balozi wao wa michezo kwa kukabidhi vifaa mbalimbali vya michezo katika muda mfupi ujao.

Kwenye ziara hiyo, Ndugu Ado aliambatana na Mwenyekiti wa Mkoa wa Kichama wa Selou Ndugu Abdallah Mtalika, Katibu Ndugu Mtutura Abdallah Mtutura, Mwenyekiti wa Jimbo Ndugu Yasini Mawila, Katibu Ndugu Francis Kavele na Katibu wa Ngome ya Wanawake Ndugu Gania Shamte.View attachment 1796440
IMG-20210524-WA0032.jpg
View attachment 1796439View attachment 1796438
 
Back
Top Bottom