Adhabu yote anayotupa hii ni ya nini? Je sisi ni majipu?

ryoba nyamhanga

New Member
Jul 11, 2016
2
1
Ndugu Rais wangu naomba nikuulize swali gumu ili unijibu nielewe. Swali langu kwako ni kwamba kwani unapotupa shida sisi vijana tuliohitimu vyuo mwaka jana tukitegemea kuajiriwa kwani sisi ni majipu?
 
Usisahau Idara na Taasisi za serikali zinaunganishwa ili kubana matumizi.Walioko makazini wenyewe matumbo joto.

Tafuta gazeti la JamboLeo la siku ya leo usome hii habari ninayokudokezea hapa.

Jiongeze.
 
Ndugu rais wangu naomba nikuulize swali gumu ili unijibu nielewe. Swali language kwako no kwamba kqani unapotupa shida sisi vijana tuliohimu vyuo mwaka jana tukitegemea kuajiriwa kwani sisi no majipu?
Umehitimu Chuo gani Mkuu, na Taaluma yako ni hipi?
 
Ndugu rais wangu naomba nikuulize swali gumu ili unijibu nielewe. Swali language kwako no kwamba kqani unapotupa shida sisi vijana tuliohimu vyuo mwaka jana tukitegemea kuajiriwa kwani sisi no majipu?

Yawezekana ukawa jipu!! Msomi makini hawezi kuandika hoja ya sentensi sita na kila sentensi ikawa na mapungufu.Tulia uandike vizuri ili ulete kitu kinachoeleweka,haraka ya nini?
 
Ndugu rais wangu naomba nikuulize swali gumu ili unijibu nielewe. Swali langu kwako ni kwamba kwani unapotupa shida sisi vijana tuliohimu vyuo mwaka jana tukitegemea kuajiriwa kwani sisi ni majipu?
Nakujibu,
Kama huwezi kujiajiri ina maana hujaelimika, na kama hujaelimika ina maana ulikuwa unapoteza muda wako na rasilimali za taifa bure ... KWA NINI USIWE JIPU!

Umesoma kozi ipi?
 
Nakujibu,
Kama huwezi kujiajiri ina maana hujaelimika, na kama hujaelimika ina maana ulikuwa unapoteza muda wako na rasilimali za taifa bure ... KWA NINI USIWE JIPU!

Umesoma kozi ipi?

Ndiyo wale wasomi wanaohimizwa kuwa na kadi za ccm ili waweze kutunukiwa vyeo!Siasa imeharibu Taifa letu,kila anayejiita msomi badala ya kuitumia Elimu yake kujitafutia ajira,anasubiri ajira za serikalini,halafu tunalazimishwa kuota ndoto za Tanzania ya viwanda,viwanda hivyo vitatoka wapi wakati kila mtu ameng'ang'ana na siasa?
 
Usisahau Idara na Taasisi za serikali zinaunganishwa ili kubana matumizi.Walioko makazini wenyewe matumbo joto.

Tafuta gazeti la JamboLeo la siku ya leo usome hii habari ninayokudokezea hapa.

Jiongeze.
Wawapunguze tu, kwani wote waliopo mitaani ni wafanyakazi wa serkila?
 
rais yupo jf..?
Hata kama Rais hayupo JF, lakini kutokana na juzi alipokuwa akiwaapisha MaDED kuwa alisoma habari ya Luhende wa Sinza kwenye mtandao wa JF, hiyo imethibitisha kuwa Rais wetu ni mpenzi mkubwa wa mtandao wa JF, kwa hiyo usitie hofu, jambo lolote utakalomuaddress Rais wetu kupitia JF atalipata direct bila kupitia kwa mtu mwingine wa kati......
 
Ndui
Ndugu rais wangu naomba nikuulize swali gumu ili unijibu nielewe. Swali langu kwako ni kwamba kwani unapotupa shida sisi vijana tuliohimu vyuo mwaka jana tukitegemea kuajiriwa kwani sisi ni majipu?[/QUOT
HAaya ndio madhara ya kwenda SHULE NA KUKARIRI badala ya kuelewa.......Wewe ebu shtuka
 
Nakujibu,
Kama huwezi kujiajiri ina maana hujaelimika, na kama hujaelimika ina maana ulikuwa unapoteza muda wako na rasilimali za taifa bure ... KWA NINI USIWE JIPU!

Umesoma kozi ipi?
NAOMBA NITOE ANGALIZO KWA KUPITIA POST YAKO: UPUMBAVU NI MZIGO

Najua ni kutafuta sifa ndio huwaongoza watu kujifanya kwamba wana akili saaaaana na wanaweza kujifanya wao wana entrepreneurship mind and successful. Hili suala la kujiajiri si geni masikioni mwangu, mara nyingi nimelisikia likielekezwa zaidi kwa vijana kutoka kwenye midomo ya wanasiasa.

Kinachonishangaza, wanasiasa hawa ni wa rika zote...wazee kwa vijana. Swali nalojiuliza: mbona wao hawajiajiri?
Nikiangalia mazingira yao, kwamba walishaajiriwa, wanakopesheka na wana uzoefu na bado hawajiajiri, wanapata wapi midomo ya kuwaambia fresh graduates wajiajiri?

Nirudi kwako wewe 'MTAKA SIFA', huyu bwana kwa mfano ndio katoka Lushoto kwenye kile chuo cha MAHAKIMU, kuna kozi au uwezeshaji gani atakuwa amepata kiasi aende akajiajiri? Au ndio domo la kukurupuka full mwendo kasi kila anayelalamika ajira tumshambulie...ndugu yetu akafungue mahakama private? Well then, kwa mtaji upi? Benki zetu hapa Tanzania zinanunua proposals?

Hebu tuache ujinga na kutafuta sifa.
 
Ndugu rais wangu naomba nikuulize swali gumu ili unijibu nielewe. Swali langu kwako ni kwamba kwani unapotupa shida sisi vijana tuliohimu vyuo mwaka jana tukitegemea kuajiriwa kwani sisi ni majipu?
Subirini viwanda vije mtapata kazi kwenye viwanda vya wachina na wahindi haya za usafi
 
Nakujibu,
Kama huwezi kujiajiri ina maana hujaelimika, na kama hujaelimika ina maana ulikuwa unapoteza muda wako na rasilimali za taifa bure ... KWA NINI USIWE JIPU!

Umesoma kozi ipi?
Kwa handwriting hiyo atakiwa
1468573479999.jpg
 
NAOMBA NITOE ANGALIZO KWA KUPITIA POST YAKO: UPUMBAVU NI MZIGO

Najua ni kutafuta sifa ndio huwaongoza watu kujifanya kwamba wana akili saaaaana na wanaweza kujifanya wao wana entrepreneurship mind and successful. Hili suala la kujiajiri si geni masikioni mwangu, mara nyingi nimelisikia likielekezwa zaidi kwa vijana kutoka kwenye midomo ya wanasiasa.

Kinachonishangaza, wanasiasa hawa ni wa rika zote...wazee kwa vijana. Swali nalojiuliza: mbona wao hawajiajiri?
Nikiangalia mazingira yao, kwamba walishaajiriwa, wanakopesheka na wana uzoefu na bado hawajiajiri, wanapata wapi midomo ya kuwaambia fresh graduates wajiajiri?

Nirudi kwako wewe 'MTAKA SIFA', huyu bwana kwa mfano ndio katoka Lushoto kwenye kile chuo cha MAHAKIMU, kuna kozi au uwezeshaji gani atakuwa amepata kiasi aende akajiajiri? Au ndio domo la kukurupuka full mwendo kasi kila anayelalamika ajira tumshambulie...ndugu yetu akafungue mahakama private? Well then, kwa mtaji upi? Benki zetu hapa Tanzania zinanunua proposals?

Hebu tuache ujinga na kutafuta sifa.

kuna katatizo hapo ...nilikopigia red...

(TWENDE WOTE KWA SAUTI YA GWAJIMA)......nakumbuka mstaafu aliestaafu kuleee akaja tena kustaafu na hukuuuuuu kisha sijui anakula maharage ya wapi yuleeeeeeee akaddai LOWASSA alimdanganya kuwa akimuunga mkono atamuajiri tena kuwa WAZIRI...akamttoa chama kileeeeeee kuleeeeeee akamleta chama hiki hukuuuuuuuu....kisha akaona ajira huku haipooooooo akarudi tena chama kileeeeee....no way MAGUFULI SHUGHULIKA NA HAWA WATU HADI WAKUELEWE.....hii ndio Tanzania tunayoitaka......no SWEAT no SWEET....
 
Ndiyo wale wasomi wanaohimizwa kuwa na kadi za ccm ili waweze kutunukiwa vyeo!Siasa imeharibu Taifa letu,kila anayejiita msomi badala ya kuitumia Elimu yake kujitafutia ajira,anasubiri ajira za serikalini,halafu tunalazimishwa kuota ndoto za Tanzania ya viwanda,viwanda hivyo vitatoka wapi wakati kila mtu ameng'ang'ana na siasa?

Kwa kweli nami niliposoma lile bandiko la mwana harakati na kada wa ccm akiwaasa wanaoitwa wasomi wa nchi hii kuhakikisha wanajiunga haraka ccm kwa mategemeo ya ajira nilistuka sana.Ajira za nchi kwa ajili ya wananchi wote wa vyama vyote na wasio na vyama kuwa za makada wa chama tawala badala ya kushindanishwa kwa wote.

Mbona kuwachagua viongozi wanaomba kura na kuchaguliwa na wote bila kujali vyama?Mbona ni hao hao makada wao tena maprofessor wakitumbuliwa wanaiuliza serikali wakafanye kazi gani?Hao ndio wasomi tunaotegemea walifanye taifa kuwa la viwanda na wavisimamie wao.Taifa la vijana wote wajasiriamali.

Hivyo viwanda vingekuwepo wangeajiriwa huko kwa idadi kubwa.Fikiria vijana wanaohitimu kila mwaka kuanzia darasa la saba,form fours,form six,vyuo vya ufundi,vyuo vinavyofundisha taaluma mbali mbali na vyuo vikuu wote waingie mitaani kwa ujasiria mali tena bila mitaji na wachache sana wakalime nao bila mikopo wala zana.

Nakubali raisi wa awamu ya tano anaweza kuwa na mipango mizuri ya kubana matumizi ili fedha zipatikane serikalini kufanya maendeleo.Ataunganisha maidara na hata wizara zenye shughuli zinazoshabihiana na maana yake ni wafanyakazi kupunguzwa na kuongeza idadi iliyopo uraiani.Lipo zoezi la kuhakiki wafanyakazi hewa linaendelea.

Litafuatiwa na zoezi la uhakiki wa vyeti vya elimu na huko nina uhakika wa kutumbuliwa robo ya wafanyakazi wa serikali na mashirika ya serikali.Wote nao watarudi uraiani.Hivyo kijana unaemuuliza raisi swali gumu kuwa utafanya nini umalizapo elimu yako anza kujipanga kuanzia sasa.Vinginevyo swali lako litaendelea kuwa gumu kwako na raisi hana jibu lako.
 
kuna katatizo hapo ...nilikopigia red... nakumbuka mstaafu aliestaafu kuleee akaja tena kustaafu na hukuuuuuu kisha sijui anakula maharage ya wapi yuleeeeeeee akaddai LOWASSA alimdanganya kuwa akimuunga mkono atamuajiri tena kuwa WAZIRI.....no way MAGUFULI SHUGHULIKA NA HAWA WATU HADI WAKUELEWE.....hii ndio Tanzania tunayoitaka

Ndio maana nikasema WANASIASA. Mimi sikumtaja mtu, ninawalenga wote wenye akili hizi za kukurupuka na maneno. Sasa sijui Magufuli anashughulika nao vipi, hebu nieleweshe!
 
Back
Top Bottom