Adhabu ya viboko mashuleni iendelee kuwepo?

Wkalala

New Member
Feb 17, 2009
3
1
Hivi Karibuni mheshimiwa Rais amesema anashangazwa vibko kuondolewa mashuleni. Anadai kwamba hata yeye alichapwa na vilimsaidia hadi sasa ni Rais. Unamsapoti? toa hoja

==================
Maoni Mengine
==================

Mambo yamebadilika sana kutokana na kuwepo kwa wanaharakati na watu wanaotetea haki za binadamu pamoja na asasi mbalimbali kuhusu adhabu ya viboko .

Adhabu za viboko enzi hizo zilikuwa ndo adhabu ambayo mwl anaridhika nayo japo enzi za utandawazi ukimpiga mtoto wa mtu kiboko kikamkwaruza hatari unayo.

Wewe kama mdau una maoni gani katika adhabu ya viboko shuleni kwa sasa?
 
Sisapoti, viboko vinafanya watoto wachukie shule. kuna aina nyingi za adhabu. hii ya physical inawafanya watoto wawe sugu.
 
Vboko n kawaida xana xema kilichoharbu mzazi cku hz ametawala mpka ofcn na daraxan pia,me naona hata maofsa elimu raisi atawaonea tu chanzo cha watoto kufeli na maadili mabovu n wazazi
 
Ndiyo nasapoti, kama walimu hawawezi kuchapa wawe wanatuita sisi wenyewe wazazi tuwe tunakwenda shuleni kuwachapa, mbona nyumbani tunawachapa na hawachukii nyumbani, unakuta mtoto analilia kurudi nyumbani hata kama ni likizo ya siku nne
 
Nasaport 100%, sababu viboko vinasaidia kushape tabia ya mtoto endapo unamwadabisha katka haki na hujamwonea, na mtoto anapochapwa aambiwe kosa na kila atapokiuka achapwe. Watoto wamekwa sugu sana, hawana maadili na hawa ni wazazi, viongozi na walez wa taifa lijalo, je kwa maadili haya wataongozaje kizazi kingine. Fimbo zirudi na wachapwe haswaa for betterment of their future.
 
Akili ya mtoto imekaa kichwani sasa kwa nini tusichape vichwa tunapachapa matako?
 
Nasapoti 100% binafsi nilivyokuwa nasoma hofu ya viboko ilinsaidia kuacha utoro, kupata wastani unaotakiwa, kuwahi shuleni, etc mwalimu alivokuwa ananigombeza hata ilikuwa haisaidii ila kwa viboko nlinyooka pale sangu high school .mbeya na nikatoka na division 2 yangu safi combination ya E.C.A
 
Akili ya mtoto imekaa kichwani sasa kwa nini tusichape vichwa tunapachapa matako?

we uduvi kwel ww kwan umesikia dawa ya vidonda hiyo unaiweka ulipoumia umeambiwa lengo la viboko ni kumuonyesha machungu akimis bihave.. mbona we ukiharisha unameza dawa kupitia mdomon kwa nn usisokomeeza unapoharishia
 
  • Thanks
Reactions: Mss
Kiboko ni kifaa pekee kinachoweza kutoa ujinga kichwani mwa mtu.
Hata Mungu alisema hilo.
Na viboka havijawahi futwa mashuleni
 
Viboko vinarekebisha tabia mitoto ya siku hizi adabu haina hata chembe si kwa wazazi, walimu hata mitaani
 
Mambo yamebadilika sana kutokana na kuwepo kwa wanaharakati na watu wanaotetea haki za binadamu pamoja na asasi mbalimbali kuhusu adhabu ya viboko . Adhabu za viboko enzi hizo zilikuwa ndo adhabu ambayo mwl anaridhika nayo japo enzi za utandawazi ukimpiga mtoto wa mtu kiboko kikamkwaruza hatari unayo, wewe kama mdau una maoni gani katika adhabu ya viboko shuleni kwa sasa?
 
Kuna walimu hawachapi bali wanapiga na hata kukudhalilisha, nasapoti adhabu ya viboko lakini isipelekee udhalilishaji na unyanyasaji, unakuta mwl anachapa fimbo miguu, mikono, mgongo mara kakupiga mateke! Binafsi kwangu mimi adhabu ya fimbo siipendi na wakati nasoma shule ya msingi na sekondari, nilikuwa sipendi fimbo coz sikuona faida ya fimbo kwani kama ni akili ninazo nyingi sana. Nakumbuka kipindi niko A'level, kuna ticha mmoja alikuwa na kiherehere sana kutufuatilia, cha ajabu itokee form two wafanye kosa hutaona akideal nao lakini ikitokea form six mkazingua, mnaona anaanza toa povu. Walimu badilikeni.
 
Back
Top Bottom