Adhabu ya mauaji ya heshima nchini Iran

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
Ni mauaji yanayofanyika na mwanafamili kwa mwanafamilia anaeyeonekana kuleta aibu au ‘laana’ katika familia au ukoo

Wanaharakati wanasema sababu za mauaji haya ni pamoja na kukataa kuolewa na kushiriki ngono nje ya ndoa, kunyanyaswa kijinsia au ubakaji

Nchini Iran mtu akipatikana kufanya mauaji haya, adhabu yake ni kati ya miaka mitatu hadi kumi jela, badala ya hukumu ya kifo

Wanaharakati wa haki za binaadamu wanasema hakuna takwimu kuhusu idadi ya mauaji haya lakini kuna ushahidi kuwa vitendo hivyo vinazidi kushamiri hasa maeneo ya mashambani

Hivi karibuni Romina Ashraf (14) aliuawa kwa kukatwakatwa na baba yake baada ya kukataa kuolewa
 
... Iran cha mtoto Mkuu; Pakistan ndio "makao makuu" ya mauwaji haya ya "honor killing". Kule vibinti vinacharangwa shingo kweli kweli na kaka zao hakuna wa kuvitetea vinajifia tu kama ndezi. Naomba niishie hapa nikiendelea zaidi watasema nawatusi.
 
Hizo ni mila za kale za watu wa Mashariki ya Kati na wameziendeleza hadi leo. Pakistan wamezinakili baada ya kuwa waislamu.

Unyama huu unaofanyika huko katika nchi zenye kukumbatia uislamu hauwezi kuongelewa na baadhi ya watu humu kwa sababu za mafungamano ya kidini na hao wauaji wa huko kwenye Islamic World.
 
Back
Top Bottom