Adhabu ya kifo haitekelezeki, Wabunge wataka ifutwe ibakie kifungo cha maisha

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,717
55,819
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imependekeza kwa Serikali kupitia upya sheria inayotoa adhabu ya kunyongwa kwa kutenga muda maalumu wa kutekelezwa na ukipita, adhabu hiyo igeuke moja kwa moja kuwa kifungo cha maisha jela.

Katika hatua nyingine, Kamati hiyo imewataja marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete kutotekeleza adhabu hiyo walipokuwa madarakani.

Mapendekezo hayo ya kamati yaliyotolewa jana na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Rashid Shangazi, yalieleza kuwa, kamati hiyo imewahi kupendekeza adhabu ya kunyongwa iangaliwe upya kwa kuwepo na muda wa utekelezaji, na kama haitatekelezwa kwa kipindi hicho, aliyehukumiwa atumikie kifungo cha maisha jela.

"Watanzania wengi wanasubiri kunyongwa magerezani, kuanzia Nyerere, hakuna tena uongozi uliotekeleza adhabu hii, Mwinyi, Mkapa, Kikwete wote hawa hawakuitekeleza, na sasa utawala huu bado haijatekelezwa, kwanini hii sheria iendelee kuwepo?" alihoji Shangazi.

Alisema aliyehukumiwa adhabuhiyo anapokaa muda mrefu gerezani, ni adhabu kubwa zaidi na anaathirika zaidi na ni kinyume cha haki za binadamu ambazo Tanzania imesaini mikataba ya Kimataifa kuzitekeleza na kuzilinda na nyingine zipo katika Katiba ya nchi.

"Kamati inashauri Serikali iangalie hii adhabu, inaweza kupendekeza katika sheria kutengwa kwa muda fulani kwa aliyehukumiwa na unapofika, automatic (moja kwa moja) inageuka kuwa kifungo cha maisha jela," ilishauri kamati.

Kamati ilishauri hayo kama mapendekezo yake ya awali kwa Wizara ya Katiba na Sheria baada ya kupitia bajeti ya wizara hiyo kifungu kwa kifungu na kuipitisha kwa maagizo ya kufanya baadhi ya marekebisho.

Mapendekezo kamili watayatoa wakati wa kuwasilisha bajeti katika Bunge linaloanza Aprili 4, mwaka huu. Juzi katika majadiliano ya wajumbe wa kamati hiyo wakati wakipitia utekelezaji wa bajeti na mpango kwa mwaka 2016/17 na mapendekezo ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2017/2018, walishauri kuwa, suala la adhabu ya kifo na mahabusu kusongamana magerezaji yatazamwe upya.

Kwa upande wake, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, aliishukuru kamati hiyo kwa mapendekezo na ushauri kwa serikali na kueleza kuwa, watayafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa kwa maslahi ya umma.

"Naomba niwahakikishie kuwa, mapendekezo yote mliotoa tumeyachukua, tutayazingatia na kuyafanyia kazi," alisema Profesa Kabudi.

Takwimu zinaonesha kuwa, Watanzania 465 wanasubiri kunyongwa katika Magereza mbalimbali nchini na tangu mwaka 1994 hukumu hiyo haijatekelezwa nchini.

Taarifa mbalimbali za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) nchini, zinabainisha kuwa, hakuna hukumu yoyote ya kifo iliyosainiwa na Rais tangu utawala wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ili kutekelezwa hadi sasa.

Ripoti ya Mpango wa Kujitathmini Kuhusu Hali ya Utekelezaji wa Haki za Binadamu (UPR), unaotekelezwa kwa mara ya pili nchini Tanzania, inaonesha kuwa hadi mwaka jana, kulikuwa na mahabusu 465 wanaosubiri adhabu ya kifo.

Kati yao wanaume ni 445 na wanawake ni 20. Wadau mbalimbali wa haki za binadamu wamekuwa wakiitaka Serikali kuifuta adhabu hiyo kwa kuwa haitekelezeki na ni kinyume cha haki ya binadamu ya kuishi ambayo pia imetamkwa katika Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, Sehemu ya Tatu, Ibara ya 14 inayosema; "Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria."

Hata hivyo, baadhi ya asasi hasa zinazohusika na haki za walemavu wa ngozi (albino), zinapinga kufutwa kwa adhabu hiyo kwa madai kuwa, hata wao wana haki ya kuishi hivyo anayewaua hana haki ya kuishi kama alivyoondoa haki hiyo kwa albino.

Kamati hiyo ilipitia vifungu kwa vifungu bajeti ya wizara hiyo ya Sh bilioni 159.3 kwa mwaka wa fedha 2017/18 kutoka Sh bilioni 191.4 mwaka 2016/17 ikiwa ni pungufu ya asilimia 4 kutokana na fedha za washirika wa maendeleo wa nje kutojumlishwa.

Chanzo: Habari leo
 
Adhabu ya kifo ifutwe na badala yake hao wafungwa waliohukumiwa kifo watumike kwenye tafiti mbalimbali za madawa na magonjwa kama vile ukimwi, Ebola, sumu ya nyoka, n.k.
 
Marehemu Jaji Msomi Mwalusanya katika kesi ya Mbushuu Mnyaroje v Republic aliwahi kulieleza vizuri sana hili swala.
 
JAJI MWALUSANYA VS HUKUMU YA KIFO.

Mwaka 1994 katika mahakama kuu mkoani Dodoma mbele ya Jaji Mwalusanya J, watu wawili Mbushuu Mnyaroje na Kalai Sungula walikutwa na hatia ya kosa la mauaji ambapo waliua mtu na kupora mifugo yake. Walikutwa na kosa la mauaji ya kukusudia (murder) kinyume na kifungu cha 196 cha Penal Code Cap 16. Walitakiwa kupewa hukumu ya kifo kwa mujibu wa kifungu cha 197 cha Penal Code, Kunyongwa mpaka kufa kwa mujibu wa kifungu cha 26 cha Penal Code.

Kabla jaji hajatoa hukumu wakili wa Mbushuu na Sungula wakili Rweyongeza aliibua hoja kuhusiana na adhabu ya kifo kwamba hukumu ya kifo ni kinyume kabisa cha katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya 1977 ibara 13(6)(d) na (e) kwa maana kwamba hukumu ya kifo ni ya kikatili,ya mateso, inayotweza utu wa mtu na isiyo ya kibinadamu. Wakili Rweyongeza alienda mbali zaidi na kusema hukumu ya kifo ni kinyume cha katiba ibara ya 14 inayotoa haki ya kuishi, kwa hoja hizo aliiomba mahakama isitoe hukumu ya kifo kwa wateja wake kwani hukumu hiyo ni unconstitutional!

Jaji Mwalusanya alikubaliana moja kwa moja na wakili Rweyongeza kwanza kwamba hukumu ya kifo ni adhabu ya mateso, kinyume cha utu na ubinadamu na ya kikatili, Jaji Mwalusanya alisema ukatili wa hukumu ya kifo unaonekana katika utekelezaji wa hukumu wake kwani si wa kistaarabu hata kidogo.

"One leading doctor described the process as slow, dirty, horrible, brutal, uncivilized and unspeakably barbaric"

Mwalusanya anasema mfungwa huachiwa umbali wa 8 feet akiwa amefungwa kitanzi shingoni lengo likiwa ni kuvunja shingo yake ili afe haraka na mara nyingine iwapo mnyongaji amemkosa mfungwa kisawasawa au shingo haijavunjika ipasavyo basi mnyongaji humpiga mfungwa risasi ya mguu au humpiga na nyundo kichwani kuharakisha kifo chake.

Mwalusanya anasema serikali inawafundisha raia kuua kwa kutekeleza hukumu ya kifo. Kama serikali inataka raia waheshimu maisha ya watu basi serikali inatakiwa iache kuua. Kama kila anayeua ni lazima naye auawe kwanini serikali isiajili wabakaji maalumu kwa ajili ya kuwabaka wale wanaobaka wengine badala yake hukumu ya ubakaji ni miaka 30 jela. Kuthibitisha kuwa hukumu ya kifo ni ya kikatili kinyume cha utu serikali inakumbwa na guilt conscience yaani inasutwa na ndiyo maana hata hukumu ya kifo hutekelezwa kwa usiri mkubwa mno.

Jaji mwalisanya anasema hukumu ya kifo ni kinyume na ibara ya 14 ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inayotoa haki ya kuishi kwa kila mtanzania. Sababu zingine ni ucheleweshwaji wa utekelezaji wa hukumu hiyo ya kifo na mazingira mabaya ambayo wafungwa wanaosubiri kunyongwa huhifadhiwa.

Jaji Mwalusanya baada ya kupinga vikali kicriticise vikali kifungu cha sheria cha kanuni ya adhabu ya makosa ya jinai (Penal Code) kifungu cha 197 na kukitangaza kuwa kinapingana na katiba yaani Unconstitutional, aliwahukumu Mbushuu Mnyaroje na Kalai Sungula kifungo cha maisha jela kila mmoja badala ya hukumu ya kifo.

Cha ajabu Mbushuu Mnyaroje na Kalai Sungula walikata rufaa kwenda mahakama ya Rufani ya Tanzania kwa sababu kwamba hawakuridhishwa na ushahidi uliotolewa dhidi yao na kwamba hawakuhusika na mauaji yoyote.

Katika mahakama ya Rufani ya Tanzania Corum ya majaji watatu ambao ni Lubuva J, Ramadhani J, na Makame J ilipokaa na kusikiliza rufaa hiyo. Majaji wa mahakama ya Rufani walijikita kwenye kuipinga vikali hukumu ya Jaji Mwalusanya, kwanza walikubaliana rufaa kwamba ushahidi hautoshelezi, pili walitengua hukumu iliyotolewa na Jaji Mwalusanya ya kifungo cha maisha kwa watuhumiwa hao badala yake waliwaachia huru Mbushuu Mnyaroje na Kalai Sungula. Pamoja na hayo walipinga vikali hoja za Mwalusanya dhidi ya hukumu ya kifo

Katika hoja zao majaji wa Rufani huku wanasema Mwalusanya alikosea kutangaza kifungu cha 197 cha Penal Code kuwa unconstitutional kwani haki ya kuishi inayotolewa kwenye katiba ibara ya 14 siyo absolute inatakiwa kuwa subjected to the law, kwa maana kwamba kila mtu ana haki ya kuishi kwa mujibu wa sheria hivyo kama ukivunja sheria haki yako ya kuishi inaondolewa kwa mfano sheria imekataza kuua hivyo ukiua haki yako ya kuishi inaondolewa kwa wewe pia kuhukumiwa kifo. Sababu ya pili ni ibara 30(2) ya katiba inayoruhusu kutotekeleza baadhi ya haki kwa mujibu wa sheria. Kwa mujibu wa mahakama ya Rufani hukumu ya kifo hutolewa kwa maslahi ya umma ili kuilinda jamii dhibi ya wauaji, kwamba jamii haipendi watu waue hivyo kuweka hukumu ya kifo ni kuilinda jamii dhidi ya mauaji.

Kwa hukumu hii ya mahakama ya Rufani ya Tanzania hukumu ya kifo inaendelea kuwa halali nchini Tanzania japokuwa in practical hukumu hii imekuwa haitekelezwi nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka 18 sasa hali ambayo imepelekea walio hukumiwa kifo kufikia zaidi ya mia nne gerezani nchini Tanzania. Hii inatokana na kelele nyingi sana kutoka kwa watetezi wa haki za binadamu na jumuiya za kimataifa.
 
Atokee kichaa asaini hati za kunyongwa wafungwa wote 400, haowezekani unapewa mamlaka na huyatumii.
Hakuna sababu ya wauaji wa albino wanapokutwa na hatia kutonyongwa.!

Sent from my TECNO P5 using JamiiForums mobile app
 
Sheria za zima moto zinazo pitishwa na wabunge wa Ccm. Kila siku kubadilishwa
 
Mbona kuna mtu alitupia uzi humu inayosema awamu ya mwinyi watu walinyongwa wengi

Kumbe ilikuwa fix
 
kwanza tuangalie nchi ambazo zinaongoza kwa kunyonga watu duniani zimeweza kupunguza uhalifu kwa kiasi gani.

na kama hizo nchi uhalifu bado upo kwa kiasi kikubwa basi inamaana kunyonga watu sio jibu lake.

na tukisema kila mtu ane uwa naye awe anauwawa. basi hata anaye baka naye awe anabakwa.
 
Bola tu wanyongwe maana wakifungwa maisha jera serikali itabidi itenge badget ya kuwalisha wao nipesa ndufu sana kwa mwaka iyo ambayo ingefanyakazi kwenye sekta mbali mbali kulikoni kuhudumia mtu ambaye not sure atatoka leo au kesho (mfugo)
 
Hivi hakuna sheria ya kumshitaki alieshindwa kutekeleza sheria tuwapeleke Mzee Ruksa Mkapa na Kikwete kwa kushindwa kwa makusudi kutekeleza majukumu yao ya kisheria?
 
Adhabu iangaliwe upya manaa wana cost kubwa kuwatunza magerezani
Nadhani hoja ya kuwalisha bure au kwa kuwa hazijatekelezwa zitakuwa nyepesi kuifuta adhabu hii. Labda hoja za implications za utekelezaji wake.
 
JAJI MWALUSANYA VS HUKUMU YA KIFO.

Mwaka 1994 katika mahakama kuu mkoani Dodoma mbele ya Jaji Mwalusanya J, watu wawili Mbushuu Mnyaroje na Kalai Sungula walikutwa na hatia ya kosa la mauaji ambapo waliua mtu na kupora mifugo yake. Walikutwa na kosa la mauaji ya kukusudia (murder) kinyume na kifungu cha 196 cha Penal Code Cap 16. Walitakiwa kupewa hukumu ya kifo kwa mujibu wa kifungu cha 197 cha Penal Code, Kunyongwa mpaka kufa kwa mujibu wa kifungu cha 26 cha Penal Code.

Kabla jaji hajatoa hukumu wakili wa Mbushuu na Sungula wakili Rweyongeza aliibua hoja kuhusiana na adhabu ya kifo kwamba hukumu ya kifo ni kinyume kabisa cha katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya 1977 ibara 13(6)(d) na (e) kwa maana kwamba hukumu ya kifo ni ya kikatili,ya mateso, inayotweza utu wa mtu na isiyo ya kibinadamu. Wakili Rweyongeza alienda mbali zaidi na kusema hukumu ya kifo ni kinyume cha katiba ibara ya 14 inayotoa haki ya kuishi, kwa hoja hizo aliiomba mahakama isitoe hukumu ya kifo kwa wateja wake kwani hukumu hiyo ni unconstitutional!

Jaji Mwalusanya alikubaliana moja kwa moja na wakili Rweyongeza kwanza kwamba hukumu ya kifo ni adhabu ya mateso, kinyume cha utu na ubinadamu na ya kikatili, Jaji Mwalusanya alisema ukatili wa hukumu ya kifo unaonekana katika utekelezaji wa hukumu wake kwani si wa kistaarabu hata kidogo.

"One leading doctor described the process as slow, dirty, horrible, brutal, uncivilized and unspeakably barbaric"

Mwalusanya anasema mfungwa huachiwa umbali wa 8 feet akiwa amefungwa kitanzi shingoni lengo likiwa ni kuvunja shingo yake ili afe haraka na mara nyingine iwapo mnyongaji amemkosa mfungwa kisawasawa au shingo haijavunjika ipasavyo basi mnyongaji humpiga mfungwa risasi ya mguu au humpiga na nyundo kichwani kuharakisha kifo chake.

Mwalusanya anasema serikali inawafundisha raia kuua kwa kutekeleza hukumu ya kifo. Kama serikali inataka raia waheshimu maisha ya watu basi serikali inatakiwa iache kuua. Kama kila anayeua ni lazima naye auawe kwanini serikali isiajili wabakaji maalumu kwa ajili ya kuwabaka wale wanaobaka wengine badala yake hukumu ya ubakaji ni miaka 30 jela. Kuthibitisha kuwa hukumu ya kifo ni ya kikatili kinyume cha utu serikali inakumbwa na guilt conscience yaani inasutwa na ndiyo maana hata hukumu ya kifo hutekelezwa kwa usiri mkubwa mno.

Jaji mwalisanya anasema hukumu ya kifo ni kinyume na ibara ya 14 ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inayotoa haki ya kuishi kwa kila mtanzania. Sababu zingine ni ucheleweshwaji wa utekelezaji wa hukumu hiyo ya kifo na mazingira mabaya ambayo wafungwa wanaosubiri kunyongwa huhifadhiwa.

Jaji Mwalusanya baada ya kupinga vikali kicriticise vikali kifungu cha sheria cha kanuni ya adhabu ya makosa ya jinai (Penal Code) kifungu cha 197 na kukitangaza kuwa kinapingana na katiba yaani Unconstitutional, aliwahukumu Mbushuu Mnyaroje na Kalai Sungula kifungo cha maisha jela kila mmoja badala ya hukumu ya kifo.

Cha ajabu Mbushuu Mnyaroje na Kalai Sungula walikata rufaa kwenda mahakama ya Rufani ya Tanzania kwa sababu kwamba hawakuridhishwa na ushahidi uliotolewa dhidi yao na kwamba hawakuhusika na mauaji yoyote.

Katika mahakama ya Rufani ya Tanzania Corum ya majaji watatu ambao ni Lubuva J, Ramadhani J, na Makame J ilipokaa na kusikiliza rufaa hiyo. Majaji wa mahakama ya Rufani walijikita kwenye kuipinga vikali hukumu ya Jaji Mwalusanya, kwanza walikubaliana rufaa kwamba ushahidi hautoshelezi, pili walitengua hukumu iliyotolewa na Jaji Mwalusanya ya kifungo cha maisha kwa watuhumiwa hao badala yake waliwaachia huru Mbushuu Mnyaroje na Kalai Sungula. Pamoja na hayo walipinga vikali hoja za Mwalusanya dhidi ya hukumu ya kifo

Katika hoja zao majaji wa Rufani huku wanasema Mwalusanya alikosea kutangaza kifungu cha 197 cha Penal Code kuwa unconstitutional kwani haki ya kuishi inayotolewa kwenye katiba ibara ya 14 siyo absolute inatakiwa kuwa subjected to the law, kwa maana kwamba kila mtu ana haki ya kuishi kwa mujibu wa sheria hivyo kama ukivunja sheria haki yako ya kuishi inaondolewa kwa mfano sheria imekataza kuua hivyo ukiua haki yako ya kuishi inaondolewa kwa wewe pia kuhukumiwa kifo. Sababu ya pili ni ibara 30(2) ya katiba inayoruhusu kutotekeleza baadhi ya haki kwa mujibu wa sheria. Kwa mujibu wa mahakama ya Rufani hukumu ya kifo hutolewa kwa maslahi ya umma ili kuilinda jamii dhibi ya wauaji, kwamba jamii haipendi watu waue hivyo kuweka hukumu ya kifo ni kuilinda jamii dhidi ya mauaji.

Kwa hukumu hii ya mahakama ya Rufani ya Tanzania hukumu ya kifo inaendelea kuwa halali nchini Tanzania japokuwa in practical hukumu hii imekuwa haitekelezwi nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka 18 sasa hali ambayo imepelekea walio hukumiwa kifo kufikia zaidi ya mia nne gerezani nchini Tanzania. Hii inatokana na kelele nyingi sana kutoka kwa watetezi wa haki za binadamu na jumuiya za kimataifa.
Nataman nipate japo kubarua cha kunyonga hao 250 kwa mwezi mmoja naweza maliza woteeee3

Dawa ya moto ni moto waliua nao wauwawe hakuna namna na wanipe waone

450/siku 30 ni sawa na 15 per day
Hahahaha so simple nipigieni debe watu wa magereza
 
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imependekeza kwa Serikali kupitia upya sheria inayotoa adhabu ya kunyongwa kwa kutenga muda maalumu wa kutekelezwa na ukipita, adhabu hiyo igeuke moja kwa moja kuwa kifungo cha maisha jela.

Katika hatua nyingine, Kamati hiyo imewataja marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete kutotekeleza adhabu hiyo walipokuwa madarakani.

Chanzo: Habari leo

Marehemu Jaji Msomi Mwalusanya katika kesi ya Mbushuu Mnyaroje v Republic aliwahi kulieleza vizuri sana hili swala.
Figga na Zawadi asanteni kwa hili.
Kwanza mimi ni miongoni mwa tunaopinga adhabu hii, ila taarifa juu ya utekelezwaji wa adhabu hii bado haiko sawa. Ilisemekana Nyerere alisaini mara moja tuu utekelezwaji wa adhabu hii kwa Mwamwindi aliyemuua kinyama Dr Cleruu.

Mwinyi, Mkapa na Kikwete wanaelezwa hawakuwahi kusaini. Soma taarifa hii ya LHRC na tujiulize ukweli ni upi?.

"KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimewataka wabunge na wadau wengine watakaoshiriki katika bunge la katiba kufuta ibara ya 69 ya rasimu inayompa rais mamlaka ya kuidhinisha utekelezwaji wa adhabu ya kifo.

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk. Helen Kijo-Bisimba alisema hayo alipokuwa akitoa tamko kwa vyombo vya habari katika maadhimisho ya siku ya kupinga adhabu ya kifo duniani.

Pia alisema tangu Tanzania ipate uhuru 1961 hadi sasa watu 238 wamenyongwa na idadi ya watu waliohukumiwa kunyongwa imeongezeka kutoka watu 46 mwaka 1961 kufikia 2562 mwaka 2007.

Nilihudhuria kongamano hili na nilishangazwa na huu ushuhuda wa mfungwa huyu aliyeelezea kushuhudia zoezi la unyongaji gereza la Isanga Dodoma!.

Siku ya Kupinga Adhabu ya Kifo

Siku ya Kupinga Adhabu ya Kifo
Unajua anaetekeleza adhabu ya kifo hufikishwa Mahakamani baada ya kazi hiyo?

Askari Mstaafu aliyekuwa ananyonga watu Gereza la Isanga-Dodoma

Adhabu ya Kunyonga Hadi Kufa imepitwa na wakati?
Magufuli shujaa, ataka 68 wa madawa wanyongwe! Kikwete alikuwa dhaifu mno, aliomba wasinyongwe!

Mhe. Rais Magufuli, Anza na Kusaini Hati za Wote Waliohukumiwa Kifo, Wanyongwe Haraka Haraka Mpaka..

Adhabu ya Kifo: Jee kweli bado inahitajika?

We really need to do something more on this.

Paskali
 
Back
Top Bottom