Baadhi ya makabila yanayo tabia ya kuwaadhibu wanaume waliowapa mimba mabinti zao. Katika jamii hizo binti akipata ujauzito, aliyechangia ujauzito huo anapigwa faini ya milioni moja. Ikiwa kama kijana huyo ataridhia kuishi na binti yao, na kupata mtoto wa pili atatozwa faini ya pili ya shilingi laki sita, wakiendelea kuishi na kupata mtoto wa tatu, atatozwa faini ya tatu ya laki nne.
Hiyo ina maanisha kijana akidhiria kwenda atapangiwa mahari, kama milioni moja na zaidi ya laki tano, pamoja na adhabu itakayotegemeana na ujauzito/idadi ya watoto. Kutokana na utaratibu huo, kijana anaweza kutozwa hata milioni tatu na zaidi ya laki tano.
Hoja yangu ya msingi ni kwamba, ikiwa kama kijana ameridhia kuishi na binti, hasa baada ya kupata ujauzito, na hata kulea watoto, je kuna haja gani ya kupigwa faini?
Sioni mantiki ya kijana kukubali kulea mjomba na shangazi kwa moyo, na anapotumia uungwana kwenda ukweni akaadhibiwa.
Mambo kama haya, kwa namna moja au nyingine, ndiyo yanayofanya vijana kutelekeza mabinti, hasa ikiwa kama kutakuwa na ushindani toka kwa binti wa kabila lenye garama nafuu za kuoa.
Inafahamika wazi kuwa mabinti, baada ya kumkubali kijana hujilengesha na kubeba ujauzito, pengine bila ya maridhiano ya kina na kijana husika, kwa lengo la kumfurahisha kijana, wala hakubakwa.
Tamaduni kama hizi za Kiafrika zinapaswa kupigwa vita.