Adha ya usafiri Dar, nani alaumiwe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Adha ya usafiri Dar, nani alaumiwe?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by TWIZAMALLYA, Oct 15, 2011.

 1. TWIZAMALLYA

  TWIZAMALLYA JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wadau mimi ni mmoja wa wahanga wa usafiri wa daladala hapa mjini. Hali ni mbaya sana kwa sasa, kwani inapofika jioni daladala nyingi zinakatisha route zake. Watu wa mbezi ya Kimara watakubaliana na mimi.Ukiwa posta mpya pale ikija dalada ya mbezi mara nyingi hawashushi abiria kituoni.Watapitiliza mbele na kuanza kushusha. Ukijidai kuikimbilia dala dala utakutana na kauli kuwa hatupakizi tunaenda gereji.Option inayokuwepo kwa mtu wa mbezi ni kupanda daladala mpaka ubungo pale napo huwezi kupata gari ya mbezi unachotakiwa ni kupanda daladala ya kimara,ukifika kimara pale utakuta gari za mbezi nyingi tu. Kwa kuangalia tu hili tatizo ni la kutengenezwa na madereva wa daladala.Hapa najiuliza hivi hawa SUMATRA kweli hawaoni hili tatizo?.Au hili si sehemu ya kazi zao na kama ni kazi zao naona hawa jamaa watakuwa wananuka rushwa sana. Maana wananipa kufikiria kuwa wenye daladala wanamchango wa hela kwa ajili ya sumatra.

  Kipindi cha MAJEMBE AUCTION MART walipopewa kazi mambo yalikuwa tofauti sana. Kwa vile daladala zote nchini zinamilikiwa na wakubwa hasa viongozi wa ccm wanaoongoza kwa uchafu hapa nchini, Majembe waliondolewa kufanya kazi ile ambayo ilikuwa inawaletea ahueni wananchi wa kawaida.Hali inazidi kuwa mbaya hakuna mtu anayejali kwa hili, hapa siongelei foleni naongelea tatizo la kukatisha ruti kwa daladala.Mfanyakazi wa kawaida kima cha chini serikalini atawezaje kumudu garama za maisha kama analazimika kupanda dala sita kwa siku kwenda na kurudi kazini?. Wakati ambapo kama serikali yake ingekuwa inamjali ingeweka angalau udhibiti kidogo kwenye eneo hili.Kuleta maisha bora kwa watu si lazima kuongeza mishahara kila wakati ni pamoja na kuweka usimamizi mzuri kwenye mambo mbalimbali yanayomhusu raia. Nadiriki kusema ccm nchi imewashinda kabisa.
   
 2. mysteryman

  mysteryman JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Magamba on action
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tuna Mayor wa Ilala, Mayor wa Temeke, na Mayor wa Kinondono. Sambamba na hili tuna Mkuu wa Wilaya - Ilala, Mkuu wa Wilaya - Temeke na Mkuu wa Wilaya - Kinondoni. Icing on the cake, tuna Mayor wa Jiji na tuna Mkuu wa Mkoa. All these posts zimetolewa kwa mfumo wa 'gentleman's agreement'. Hawakuchaguliwa na wananchi na hivyo hawawajibiki kwa wananchi. Ndio maana ni muhimu sana kuwa na katiba mpya itakayorudisha mamlaka kwa wananchi.
   
 4. Ze burner

  Ze burner JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 460
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  kama jiji limekushinda hama coz yajayo mbele ni makubwa zaidi.
   
 5. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Wapi MWAIBULA?
  Mnamkumbuka? huyu alikuwa kiboko yao.
   
 6. S

  SIKUOGOPI Member

  #6
  Oct 15, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pambafuuuuuuuuu! Mbona umechelewa!
   
 7. Kitty Galore

  Kitty Galore JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 347
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kachelewa wapi?
   
 8. TWIZAMALLYA

  TWIZAMALLYA JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nitakuwa nime solve matatizo?, umejuaje yajayo ni makubwa au na wewe uko kwenye Nec ya ccm mnapanga strategies jinsi ya kutafuna nchi. maana hatujajua mpaka sasa mtakuwa na issue gani ya kuleta kiama mnaojua ni nyinyi tu ndio maana unaweza ukasema with certainity kwamba yajayo ni makubwa.
   
 9. Mageuzi

  Mageuzi Member

  #9
  Oct 17, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usafiri wa Majiji yote makubwa duniani huwa na operators wachache.e.g london kuna kampuni 5 tu za daladala.na zote zinapewa route na halmashauri ya jiji la london.
  kwetu sisi UDA ingepewa mamlaka ya route za Dar.alafu ikatoa tenda kwa makampuni ili usimamizi wa maderava na magari uwe makini zaidi.
  cha kushangaza sasa Dar kuna usafiri wa Bajaji,Bodaboda hadi samora.ikumbukwe hizi pikipiki wamiliki wengi ni maofisa wa serikali,itakuwa ngumu kuzidhibiti kama ilivyo ngumu kudhibiti dala dala zinazomilikiwa na maofisa waandamizi na wakurugenzi wa serikali.
   
 10. Ze burner

  Ze burner JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 460
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  hii mzee haihitaji uwe ndani ya kamati kuu ya magamba hali yenyewe tu inatabiri
   
Loading...