Adha kutoka namba ya simu 0901655670

Adha kutoka namba ya simu 0901655670

Faana

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
43,274
Reaction score
51,692
Ndugu zangu wanajamvi, nimekuwa napigiwa simu na namba tajwa 0901655670 ambayo kwangu naona ni karaha kwa sababu ujumbe ninaopewa siyo sehemu ya mahitaji kwenye yangu, ninaamini tupo wengu humu tunaosumbuliwa na namba hiyo, nadhani ipo haja sasa mamlaka husika (TCRA) kutoa amri kwa mtoa huduma kusitisha mara moja usumbufu huo kwakua inaingilia majukumu ya watu na kuwapotezea muda.

Kama ni matangazo ya biashara, mimi nitayatafuta kwa wakati wangu kwenye mtandao, au kwenye mabango barabarani na siyo kunibandikia kwenye kuta za nyumba bila ridhaa - nawasilisha
WhatsApp Image 2018-09-25 at 18.08.34.jpeg
yangu
 
Yaani wanakera mnoo mkuu" Afadhali umepaza sauti hapa" huwenda itasaidia wao kujirekebisha


Watumishi wanaambiwa wasitumie mitandao ya kijamii muda wa kazi, je hawa si nao wanatenda kosa kwa kupeleka maudhui ambayo siyo preference kwa wateja?
 
Wameona SMS zao hatusomi wamekuja na njia ya kutupigia.

Walimpigia bibi yangu akasema ndio "Firimasoni" hawa.

Ni adha sana hizi calls.
 
Ndugu zangu wanajamvi, nimekuwa napigiwa simu na namba tajwa 0901655670 ambayo kwangu naona ni karaha kwa sababu ujumbe ninaopewa siyo sehemu ya mahitaji kwenye yangu, ninaamini tupo wengu humu tunaosumbuliwa na namba hiyo, nadhani ipo haja sasa mamlaka husika (TCRA) kutoa amri kwa mtoa huduma kusitisha mara moja usumbufu huo kwakua inaingilia majukumu ya watu na kuwapotezea muda.

Kama ni matangazo ya biashara, mimi nitayatafuta kwa wakati wangu kwenye mtandao, au kwenye mabango barabarani na siyo kunibandikia kwenye kuta za nyumba bila ridhaa - nawasilishaView attachment 877645yangu
Mimi pia ni mhanga wa hii kero..!
 
Back
Top Bottom