Adha karibu na geti la Ikulu Dar!

Adha karibu na geti la Ikulu Dar!

Barabara ya kutokea jet lumo kwenda buza jamani ina mashimo mengi kama sio ya lami bhana....
Juzi nimepita hiyo njia nilijuta maana si kwa mashimo yake. Wakandarasi wengine wa aina waliojenga barabara ile wanapaswa kufutiwa leseni kabisa wapewe za kujenga njia za miguu kwenye mbuga za wanyama.
 
Jamani namii niseme,Buguruni mnyamani Vingunguti kuibukia barakuda daaah nmeacha gari aisee, hv yale mahandaki inakuwaje jamani serikali ya mtaa ipo kweli najuta nimepita juzi had nikahisi homa
 
Jaman na mm huku Barabara ya MPITIMBI kwenda LITAPWASI huku SONGEA vijijin BARABARA ina mashimo sana ipo chini ya TANROAD tunaomba mtuone na sisi samahan sana naona wengi wanaocoment ni wa BARABARA za darisalamu samahan kwa kuingilia Uzi
 
Huu uzi kila mtu anataja eneo analokaa au sehem karibu na hyo anapopita kila siku hvyo ni rahisi kuwatia kwenye visafleti
 
Namimi niseme barabara ya sinza makaburuni kama unaelekea sam nujoma road(igesa road) inawekwa viraka kila mara lakini mashimo yamerudi vilevile.


Viraka ni vingi kuliko lami ya awali, kuna mtu alisema ukiziba viraka vidogovidogo inakuwa ngumu kugawana 10% kwakuwa ni kasungura bora kusubiri tembo
 
Huu uzi kila mtu anataja eneo analokaa au sehem karibu na hyo anapopita kila siku hvyo ni rahisi kuwatia kwenye visafleti


Kama wapo kwa ajili ya wanyonge basi huu uzi ni msaada kwao kujua wapi wakafanye kazi, sina uhakika kama Tanroads wana kitengo cha ku survey barabara wanazohudumia, vinginevyo itakuwa kama yule mtoto wa shule aliyemuarifu Rais kuhusu ukosefu wa choo cha shule kule Morogoro
 
Mimi nina shimo kubwa la mfuko wa suruali, naamini hili si tatizo langu peke yangu. Ikulu walitazame hilo.
 
endeleeni tu kusema
onyo asije mtu kusema anasimo ktk ya makalio yake....... nitamziba mimi asisubiri serikali
 
Jamani na sisi wa kivule huku Barabara hovyoo mashimo kila kona daraja limeharibika,magari hayafiki twatembea kwa mguu
 
Na mimi ngoja niseme jamani mahandaki yaliyopo barabara ya kuingia kituo cha mabasi cha Simu 2000 a.k.a Mawasiliano wahusika hamuyaoni? Sio haki kabisa barabara ni mbovu kupita maelezo na hii imesababisha hata mule ndani ya kituo kumejaa tope utadhani kuna maandalizi ya kutengeneza matuta ya bustani ya mchicha.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] mahandaki!!!![emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Huku kwetu sio mashimo ya mvua....wanachimba kbs mashimo makubwa...sielewi kwnn...pumbafu tnapata shida tu
 
Na mimi niseme, mashimo makubwa yanayotia aibu yapo Azikiwe road nje ya ILO offices, kwenye geti la ILO kabisa mashimo yametapakaa barabara nzima hamna hata pa kukwepea.

Aisee hilo shimo ni kubwa mno! Virtz inaweza ikapotelea ndani na isionekane mazima!
 
Jamani namii niseme,Buguruni mnyamani Vingunguti kuibukia barakuda daaah nmeacha gari aisee, hv yale mahandaki inakuwaje jamani serikali ya mtaa ipo kweli najuta nimepita juzi had nikahisi homa
yaaani huku hakufai kabisaa hao wengine wanalalamika lakini vingunguti aaaah nilijuta kupita huko. barabara nzima ni mahandaki tu.
 
Kampuni ya ujenzi tanora sijui imejenga kibarabara mwenge nzasa yani wameleta matope hatari hapapitiki nimepanga niite clouds na itv wawatangaze
 
Na mimi ngoja niseme jamani mahandaki yaliyopo barabara ya kuingia kituo cha mabasi cha Simu 2000 a.k.a Mawasiliano wahusika hamuyaoni? Sio haki kabisa barabara ni mbovu kupita maelezo na hii imesababisha hata mule ndani ya kituo kumejaa tope utadhani kuna maandalizi ya kutengeneza matuta ya bustani ya mchicha.
Aisee, hii njia yaweza kuwa njia mbaya kuliko zote kwenye majiji ya Tanzania!
 
Pia barabara ya kutoka Mwenge kupita lugalo kwenda tegeta, ingawa ni lami, ila ukifumba macho wakati umepanda gari na linapita hiyo barabara unaweza sema mnapita kwenye bumps zisizoisha!
Wajenzi wa hizi barabara hovyo sana.
 
Aisee, hii njia yaweza kuwa njia mbaya kuliko zote kwenye majiji ya Tanzania!
Hivi inakuaje wanajenga kituo kizuri alafu barabara ya kuelekea hapo kituoni ikawa vile??
Nahisi kuna watu wamekula hela maana nyumba za jirani zina alama za X ila ni kitambo sasa.
 
Mashimo karibu na geti la IKULU ya Magogoni yamerudi. Hiii ni aibu kwa sehemu nyeti kama ile kuwa mbovu kiasi kile.

Hivi wahusika hawapaoni?

Halafu ile fensi ya ikulu pamoja na garden ya pembeni vinatia aibu sana. Fensi ina fangasi balaa! Kuna mateja hapo fery hawana kazi. Wapeni hata kazi ya kuosha hiyo fensi

Aahhh!


Kuna mashimo makubwa sana kwenye barabara ya kutokea Ferry hapa Dar karibu na geti la Ikulu yanasababisha foleni sana.

Wahusika kama watapata hizi taarifa tafadhali sana watuwekee hata mawe madogo madogo ili kupunguza hii kero. Mtu unatumia dkk 10 nzima pale sababu ya hayo mashimo.

Regards
Jimmy

Updates: Wahusika naona wameshachukua hatua.

Bado pale karibu na geti la kuingia soko la samaki ferry dsm.
 
Back
Top Bottom