Adha karibu na geti la Ikulu Dar!

Adha karibu na geti la Ikulu Dar!

Jimmy Romio

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
367
Reaction score
278
Kuna mashimo makubwa sana kwenye barabara ya kutokea Ferry hapa Dar karibu na geti la Ikulu yanasababisha foleni sana.

Wahusika kama watapata hizi taarifa tafadhali sana watuwekee hata mawe madogo madogo ili kupunguza hii kero. Mtu unatumia dkk 10 nzima pale sababu ya hayo mashimo.

Regards
Jimmy

Updates: Wahusika naona wameshachukua hatua.

Bado pale karibu na geti la kuingia soko la samaki ferry dsm.
 
Kwakua umesema, nami niseme pale jirani na kwa kakobe kona ya kuelekea Mori kuna bonge la shimo yaani aibu. Shimo hilo limekuwa likifukiwa linaibuka tena ndani ya wiki. Wahusika nadhani kipindi cha mvua ndo muda mzuri wa kufanya utafiti lakini hawaonekani.

Jamani wekeni kero zote hapa za barabarani!!
 
Nami nasema, shimo lolilopo barabara ya morogoro uelekeo wa kimara katikati la lami karibu na kituo cha mabasi mwendokasi Kona, ni kero hasa nyakati hizi za mvua. Shimo halionekani hivyo watu wanakuja wamejiachia kisha unashangaa PAAAH, ingawa wahusika wamejaribu lifunia ila bado lipo lipo. Ni katikati ya barabara ya lami.
 
Na mimi ngoja niseme jamani mahandaki yaliyopo barabara ya kuingia kituo cha mabasi cha Simu 2000 a.k.a Mawasiliano wahusika hamuyaoni? Sio haki kabisa barabara ni mbovu kupita maelezo na hii imesababisha hata mule ndani ya kituo kumejaa tope utadhani kuna maandalizi ya kutengeneza matuta ya bustani ya mchicha.
 
Na mimi nasema, barabara ya Chuo kikuu kama unatokea Msewe au Changanyikeni imejaa mashimo. Hii barabara ndio inasababisha foleni asubuhi na jioni.
Mnaohusika fanyeni kazi na sio kujaza mchanga siku mbili shimo linarudi tena.
 
ukiona hivyo sio kwamba wenyewe wameshindwa kutengeneza nahisi labda wanataka mkereke na msipite huko tu, ni hisia zangu tu inaweza nisiwe sahihi...
 
Na mimi ngoja niseme jamani mahandaki yaliyopo barabara ya kuingia kituo cha mabasi cha Simu 2000 a.k.a Mawasiliano wahusika hamuyaoni? Sio haki kabisa barabara ni mbovu kupita maelezo na hii imesababisha hata mule ndani ya kituo kumejaa tope utadhani kuna maandalizi ya kutengeneza matuta ya bustani ya mchicha.

ndani ya kituo kumejaa tope utadhani kuna maandalizi ya kutengeneza matuta ya bustani ya mchicha
 
Na mimi ngoja niseme jamani mahandaki yaliyopo barabara ya kuingia kituo cha mabasi cha Simu 2000 a.k.a Mawasiliano wahusika hamuyaoni? Sio haki kabisa barabara ni mbovu kupita maelezo na hii imesababisha hata mule ndani ya kituo kumejaa tope utadhani kuna maandalizi ya kutengeneza matuta ya bustani ya mchicha.
Hahahaa et matuta ya mchicha. Viongozi jitahidini kurekebisha hizo kasoro zinazoelezwa ili kuepuka mifano inayofurahisha. Hahahaa
 
Na mimi ngoja niseme jamani mahandaki yaliyopo barabara ya kuingia kituo cha mabasi cha Simu 2000 a.k.a Mawasiliano wahusika hamuyaoni? Sio haki kabisa barabara ni mbovu kupita maelezo na hii imesababisha hata mule ndani ya kituo kumejaa tope utadhani kuna maandalizi ya kutengeneza matuta ya bustani ya mchicha.
Kwa nn wasiwekw lami tu
 
Ubovu wa hiyo barabara unapelekea hata kituo chenyewe kwenye lane ya entry kujaa tope zito utadhani hamna tarmac! Hii barabara ni kero haswa, inanikumbusha kituo cha daladala mwenge zamani na yale mahandaki.
 
Namimi niseme barabara ya sinza makaburuni kama unaelekea sam nujoma road(igesa road) inawekwa viraka kila mara lakini mashimo yamerudi vilevile.
 
Kwani Manispaa ya Ilala hawayaoni Yale mashimo pale KINYEREZI SHULE yanasababisha foleni asubuhi na jioni kwa watumiaji wa Barbara ya Kinyerezi-Mbezi
 
Nami niseme Kigamboni kibada corner stone kuna handaki haswa wahusika tutoleeni kero hii
 
Subirini flyover, SGR, Stiggler's, Dreamliners, na mengineyo yakamilike, mashimo ni vitu vidogo vitashughulikiwa muda wake ukifika.
 
Na mimi niseme, mashimo makubwa yanayotia aibu yapo Azikiwe road nje ya ILO offices, kwenye geti la ILO kabisa mashimo yametapakaa barabara nzima hamna hata pa kukwepea.
 
Barabara ya kutokea jet lumo kwenda buza jamani ina mashimo mengi kama sio ya lami bhana....
 
Nami niseme, kuna shimo kubwa kwenye mteremko eneo la Segerea gerezani kama unateremka kuelekea Kinyerezi. Hili eneo kuna kampuni inaitwa SCOL ndo chimbo lake la pesa. Kila baada ya mwezi utawaona wanatengeza. Baada ya wiki mbili mashimo yanarudi upya. Sijui wanafukia juu wanaacha maandaki chini ili kesho waitwe tena?
 
Back
Top Bottom