sikijui kipindi chake cha uchezaji pale klabu ya simba alikimaliziaje ,yaani alistaafu, alifukuzwa au alihamia klabu nyingine, lkn nafahamu akiwa katibu mkuu wa klabu ya simba alianza porojo kama anavyofanya sasa , simba ilienda Brazil ziara ya mafunzo siku 45, iliporudi iliingia kwenye ligi na ilianza na CDA kule DODOMA washinda 3-0 , mechi ya pili walicheza na tumbaku morogoro wakashinda 4-0 , mechi ya tatu wakakutana na yanga matokeo yakawa 0-0. marudiano raundi ya pili simba akapigwa 3-1, simba wakianza kufunga mfungaji akiwa marehemu Mussa kihwelu, goli la kusini uwanja wa zamani taifa , magoli ya yanga yakifungwa na Charles Boniface Mkwasa goli la kaskazini kisha makumbi Juma [homa ya jiji] goli la kaskazini na Omari hussein [keegan] akiitimisha karamu ya mabao. baada ya hapo porojo za Rage zikaanza kushtukiwa matokeo ya timu yakawa hovyo , wanachama wakachachamaa akang'olewa ukatibu mkuu, leo hii simshangai mtu huyu hajabadilika ni mtu mwenye porojo mf; anasema ule waraka aliopelekewa na wanachama wanaotaka mkutano wa dharura, kwa kuwa haujakamilika basi kisheria unakuwa hauna maana sawa na toilet paper jiulize mkataba wa simba na kelvin yondan ulikuwa na mapungufu viongozi wa tff walimwambia hivyo2 kuwa ni sawa na toilet paper ila yeye akawa anatoa porojo kwa wana simba . hakika Rage ni shabiki si kiongozi wa hadhi ya mwenyekiti leo hii masuala ya simba anaenda kuyapanga mwenyewe huko mjini Tabora.