DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Chama cha Alliance Democratic Change (ADC) kimeungana na viongozi wa juu wa nchi kulaani vikali vitendo vya utekaji vinavyoendelea kushamiri katika baadhi ya maeneo nchini, vikihusisha raia wa kawaida, watoto, na hata wanasiasa.
Akizungumza Juni 29, 2025, katika Mkutano Maalum wa chama hicho wa kuchagua wagombea wa nafasi za Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Urais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa ADC, Shaban Itutu, amesema utekaji ni vitendo vya aibu na vya kuvunja misingi ya utu na amani ya taifa.
Itutu amesema watu wanaojihusisha na vitendo hivyo hawawezi kuwa salama, kwa kuwa damu ya mtu haijawahi kumuacha yeyote akiwa salama. Amesema utekaji unaonesha upungufu mkubwa wa maadili na hofu ya Mungu.
Mwenyekiti huyo ametumia jukwaa hilo pia kuunga mkono kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyekemea vikali matukio ya utekaji, akisema ADC ipo tayari kushirikiana na serikali kuhakikisha Tanzania inabaki kuwa nchi ya amani.