Adabu ya mke kwa Mumewe (1): Sifa 10 ambazo mumeo anahitaji kuzisikia kutoka kwako

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
SIFA 10 AMBAZO MUMEO ANAHITAJI KUZISIKIA KUTOKA KWAKO




Chukua moja katika sifa na pongezi hizi 10 na umfurahishie mumeo leo.

Vitu na mambo tunayoyasema yana athari kubwa kwenye ndoa zetu. Wakati fulani wanaume hujulikana kwamba ni wachache wa kuwasiliana kimahabba, lakini hilo halina maana kwamba hawahitaji maneno matamu na yaliyojaa pongezi kutoka kwa wake zao. Hata kama mumeo hakwambii kuwa anahitaji maneno matamu ya kimahabba, nimeamua nikuletee sifa na pongezi kumi ambazo mumeo anahitaji kuzisikia.

1. NINA FURAHA SANA KUOLEWA NAWE

Wanaume wanahitaji kuhisi kuwa wako salama katika ndoa, na njia ya haraka kabisa ya kumuonesha mumeo kuwa yeye ndo kakalia kiti cha enzi cha moyo wako ni kumwambia ana kwa ana. Hii ni sifa na pongezi kubwa kwa sababu inaweza kutoka kwa hiari bila mumeo kutumia nguvu kuipata. Sifa na pongezi ya papo kwa papo huleta hisia ya uhalisia na ikhlasi.

2. NINAPENDA UNAVYOIHUDUMIA FAMILIA YAKO

Wanaume wanachukua jukumu kubwa katika kuhudumia familia, na wanahitaji juhudi zao zitambuliwe. Mfanye mumeo atambue kuwa sio lazima atafute mamilioni ya pesa kukufurahisha, bali hata hicho kidogo anachowaletea kinakufurahisheni.

3. UNANIFANYA NIJIVUNIE

Utafika mbali katika ndoa yako ukiwa shabiki namba moja wa mumeo. Wakati watu wakijaribu kumshusha na kumuangusha, jitahidi uwe mtu unayempandisha na kumpeleka kileleni.

4. WEWE NI BABA BORA

Kama mna watoto, msifu mumeo kwa namna anavyojihusisha na familia yake. Mfanye atambue kuwa yeye ni nguzo muhimu ya familia yenu.

5. UNANIVUTIA SANA

Mumeo anahitaji kujua kuwa unaupenda muonekano wake, hata kama ndoa yenu ina miaka mingi. Wanaume wengi hutuma na kupokea upendo kupitia ukuruba wa kimwili, hivyo kuusifu mwili wake ni miongoni mwa njia za haraka sana za kumuonesha upendo katika namna anayoielewa kabisa.

6. AHSANTE KWA KUREKEBISHA KITASA

Mumeo anaposhiriki kazi ndogo ndogo za nyumbani, msifu kwa juhudi zake. Anahitaji kuhisi kuwa anaweza, hasa pindi anapojitahidi kuwapatia huduma.


7. AHSANTE

Anapokusaidia baadhi ya mambo mshukuru.. hilo litampa nguvu na kumfanya ajitume zaidi na usimtishe kwa kumkatisha tamaa.

8. DAIMA UNAWEZA KUNICHEKESHA

Mfanye atambue kuwa anakufurahisha na kuleta nishati maridhawa ndani ya nyumba. Hata kama mumeo si mcheshi, bado unaweza kumsifu ili kumpa hamasa.

9. WEWE NI IMARA

Ikitokea mumeo akanyanyua kitu kizito, mtazamo kwa jicho la huba na umsifu kwa nguvu zake, hata kama ungeweza kuifanya kazi hiyo wewe mwenyewe. Wanaume wanahitaji kujua kuwa wanaweza kufanya mambo, na wanahitaji kujua kuwa wana msaada mkubwa kwako.

10. NINAPENDA KUKAA PAMOJA NAWE

Sote tunakuwa na majukumu mbalimbali yanayotubana kila siku katika maisha yetu, hivyo mfanye mumeo ajue kwamba bado unapenda kukaa pembezoni mwake. Hakika, wewe ni rafiki yake bora na swahiba wa maisha yake.

Tumia angalau muda wako kidogo kumshukuru mume wa maisha yako kwa yote anayoyafanya. Haikugharimu kumfurahisha mumeo, ipandishe morali yake na umfanye atamani kukunyanyua.
 
Back
Top Bottom