sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,325
- 2,491
Serikali ilitangaza kutoa ada elekezi kwa shule za watu binafsi ili kupunguza gharama kubwa wanazotozwa wazazi wanaosomesha watoto wao katika shule hizo.
Zamani ilikuwa watoto wanaofaulu kwenda sekondari, walisoma sekondari za serikali na zile za binafsi walienda kusoma wale waliokosa alama za juu za kujiunga na shule hizo. Uvurugaji ulipokuja, ikawa kinyume chake kuwa wanaopata alama za juu husoma sekondari za binafsi na wenye alama za chini na wazazi wao kuwa na kipato kidogo ndio husoma za serikali. Ni vema hadhi ya shule za serikali ikarudi kwa kuzibana shule binafsi maana wameifanya elimu kuwa biashara na siyo huduma.
Zipo shule za awali na sekondari katika mhula huu licha ya shule za serikali kufuta ada na michango, wao wamepandisha ada na michango zaidi. Hali ya utoaji elimu katika baadhi ya shule siyo nzuri.
Mfano kuna shule moja hapa Arusha mtoto wa darasa la tatu mbali na ada kupanda, anahitaji kwenda na kaunta book 19 ambapo ana masomo 12, na hayo 6 ni ya majaribio na mazoezi na moja ni la akiba. Sijui shule zingine ila je mtoto huyu ambaye hata miaka 10 hana ataweza kumudu masomo yote hayo? Mfumo wa utoji elimu ni rafiki kwa watoto?
**Raisi wetu ada elekezi tafadhali.
**Waziri wa Elimu mitaala rafiki ya Elimu tafadhali
Nawasilisha