DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Dodoma, kimesimamisha Wagombea wa Ubunge katika Majimbo tisa katika Mkoa wa Dodoma, likiwamo Jimbo la Mtumba na Madiwani Themanini na nane katika ya Kata za Majimbo hayo ambapo Septemba 4, 2025 kinatarajia kuzindua kampeni zake za kuanza kunadi wagombea wao katika maeneo mbalimbali ya Majimbo Hayo
Akizungumza Jijini Dodoma Mwenyekiti wa Chama Cha ACT Wazalendo Bw. Yohana Mussa, amesema watazindulia kampeni zao katika eneo la Zuzu Jijini Dodoma na kufuatiwa na Kata za Mtumba, Madukani, Kizota, Chang'ombe na Ipagala ambapo amewataka wananchi wa Vyama vyote kujitokeza kusikiliza Sera zao.