GE2025 ACT Wazalendo Wasilisha Maelezo kwa Msajili Kuhusu Malalamiko ya Uteuzi wa Luhaga Mpina kuwa mgombea wa urais

GE2025 ACT Wazalendo Wasilisha Maelezo kwa Msajili Kuhusu Malalamiko ya Uteuzi wa Luhaga Mpina kuwa mgombea wa urais

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Chama cha ACT Wazalendo kimewasilisha maelezo kwa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kikieleza msimamo wake kuhusu malalamiko yaliyotolewa na Katibu Mwenezi wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Monalisa Joseph Ndala, kupinga uteuzi wa Luhaga Joelson Mpina kuwa mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2025.

Malalamiko hayo yaliwasilishwa kwa Msajili kupitia barua ya tarehe 14 Agosti 2024, ambapo Monalisa ambaye pia ni Naibu Waziri Kivuli wa Sanaa, Utamaduni na Michezo katika Baraza Kivuli la Mawaziri la ACT-Wazalendo, alidai mchakato wa uteuzi wa Mpina ulikiuka Kanuni za chama na Sheria ya Vyama vya Siasa.

Katika hoja zake, Monalisa alibainisha kwamba Mpina hakukidhi matakwa ya kanuni za chama ikiwemo kuwa mwanachama kwa angalau mwezi mmoja kabla ya kuteuliwa, kutangaza mali zake binafsi, na kuonesha uelewa wa falsafa na sera za ACT-Wazalendo. Aidha, alidai kwamba mabadiliko ya kanuni za mwaka 2024 yanamtaka mgombea kuwa mwanachama kwa siku saba kabla ya mchakato wa uchaguzi wa ndani kuanza, jambo ambalo kwa mujibu wake Mpina hakutimiza.

Soma Pia: Msajili wa Vyama Vya Siasa apokea malalamiko dhidi ya mchakato wa Uteuzi wa Mgombea Urais ACT-Wazalendo

Msajili wa Vyama vya Siasa kupitia barua iliyosainiwa na Sisty Nyahoza tarehe 19 Agosti 2025, aliitaka ACT-Wazalendo kutoa maelezo juu ya malalamiko hayo kabla ya tarehe 20 Agosti 2025 saa tisa na nusu alasiri, kwa kuzingatia ratiba ya uchaguzi iliyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).

Hata hivyo, vyanzo vyetu vya kuaminika kutoka ndani ya ACT vimeeleza kuwa hoja za Monalisa zimejengwa juu ya kanuni zilizofutwa. Kwa mujibu wa chama hicho, Kanuni za mwaka 2016 ambazo zilikuwa na sharti la mwanachama kutumikia kwa mwezi mmoja, kutangaza mali na kuonesha uelewa wa falsafa ya chama, zilifutwa rasmi mwaka 2024. Badala yake, ACT kwa sasa inatumia Kanuni za Uendeshaji za mwaka 2024 na Mwongozo wa Uchaguzi wa mwaka 2020, ambazo zinamtaka mgombea kuwa mwanachama angalau ndani ya siku saba pekee kabla ya kuanza kwa mchakato wa uteuzi wa wagombea uongozi wa serikali, na kwamba sharti alilolieleza Monalisa lilihusu wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya chama.

Kwa msingi huo, chama kimeeleza kuwa uteuzi wa Mpina ulifanyika kwa mujibu wa kanuni halali zilizopo, na hivyo hakukuwa na uvunjifu wa masharti.
 
Back
Top Bottom