We Mzee acha kujipendekeza...nenda Lumumba mkasovu issue zenuChama cha ACT-Wazalendo kimesema hakitashiriki uchaguzi katika majimbo ya Kinondoni na Siha kwa kuwa sababu zilizowafanya wasusie uchaguzi mdogo uliopita, bado hazijafanyiwa kazi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 21, 2018 Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho-Bara, Msafiri Mtemelwa amesema changamoto walizozilalamikia katika uchaguzi wa Januari 13 katika majimbo ya Singida Kaskazini, Songea Mjini na Longido bado hazijafanyiwa kazi.
Amesema bado chama hicho kitaendelea kushinikiza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kufanya mageuzi katika mchakato wa uchaguzi.
Amesema malalamiko ya chama hicho kwa NEC ni matumizi ya nguvu ya vyombo vya dola dhidi ya vyama vya upinzani kwa lengo la kukisaidia chama tawala CCM.
Uchaguzi wa Siha na Kinondoni unafanyika baada ya waliokuwa wabunge wa majimbo hayo kuhamia CCM Desemba mwaka jana.
Chanzo: MCL
Kwani pato linaenda kwenye chama au serikalini?Hivi CHADEMA wanadhani CCM itawaachia jimbo la Kinondoni kiurahisirahisi tu?.
Kinondoni ndo jimbo lenye Pato kubwa kuliko jimbo lolote nchini.
Hawana hela, trust me. Hawana hela na chama kimepukutishwa sana. Wanarudi kujipanga upya. Hata hivyo majimbo ya Dar sio priority yao. Ingekuwa ni moja ya majimbo ya Kigoma Zitto angewakopesha pesa na Magari yake. Mimi nipo ACT kimaslahi ingawa moyoni ni CDM Damu, niamini, ACT WamefuliaWangewasiliana na chadema, maana inashiriki, inawezekana changamoto walizopigia kelele tume imezifanyia Kazi.
Ni imani yangu kwenye chaguzi hizi mbili ,za Kinondoni na Siha, chadema ikitokea wakashindwa, watakua wameshindwa kihalali na hakutakua na visingizio vyovyote vile, kwani wameingia wakiamini kila kitu tume ya uchaguzi imekifanyia kazi
Kwani Chadema wanazitoa wapi?!Hawana hela za Kampeni wasituzingue
Kuna chama gani cha kuishinda ccm kwenye huo uchaguzi.ACT hawawezi kushinda, wasitafute huruma.
NEC: Chama cha Siasa kutangaza kugomea uchaguzi hakuwezi kuifanya Tume iuahirishe! Tume haiko kushawishi chama kushiriki