real G
JF-Expert Member
- Feb 7, 2013
- 5,227
- 5,287
DAR: Chama cha ACT Wazalendo kimesema hakitashiriki uchaguzi mdogo wa Wabunge na Madiwani uliopangwa kufanyika tarehe 17 Februari kutokana kuwepo kwa kasoro nyingi uchaguzi uliopita na Tume ya Uchaguzi kutozunguzumzia kasoro hizo
Wakiongea na waandishi wa habari leo, Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo bara, ndugu Msafiri Mtemelwa na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma, ndugu Ado Shaibu wamesema Tume ya Uchaguzi ilikutana na wadau na kuzungumza nao na kukiri baadhi ya kasoro kwenye uchaguzi mdogo uliopita na kuwakemea Wakuu wa Wilaya na Mikoa kutoshiriki katika kampeni za uchaguzi
Ila tume hiyo haijakemea kasoro nyingine zilizojitokeza kama matumizi ya vyombo vya dola ambavyo vimekuwa viliwatisha wananchi na kuwapiga wakati wa uchaguzi
Naibu Katibu huyo amesema alishuhudia kwenye uchaguzi uliofanyika kata ya Muungano huko Urambo Tabora polisi wa FFU wakiwa wengi kupita kiasi kitu ambacho anasema kinawaogopesha watu kutoshiriki
Amezungumzia pia Chama tawala (CCM) kiliwatumia Wakurugenzi wa Halmashauri walioteuliwa na Rais kwa kuzingatia Ukada ili kushinda uchaguzi
Ameendelea kusema baada ya mbinu zote kushindwa chama tawala kilijitangazia ushindi na tume kutojali kabisa malalamiko