ACT-WAZALENDO wamsimamisha uanachama Mgombea Urais wa Zanzibar

Hansen Nasli

JF-Expert Member
Mar 18, 2012
883
337
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUSIMAMISHWA UANACHAMA NDUGU KHAMIS IDD LILA
NA NDUGU ALI MAKAME ISSA

Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT - Wazalendo) katika kikao chake cha Kamati Maalum ya Zanzibar cha tarehe 19 Februari, 2016 kimepokea taarifa rasmi kuwa aliyekuwa mgombea wa urais wa zanzibar ndugu Khamis Idd Lila kwa kushirikiana na ndugu Ali makame Issa huku wakitambua msimamo wa Chama kwa makusudi wameamua kupingana na msimamo huo kwa maslahi yao binafsi na kukidhalilisha na kuingiza mgogoro usiokuwa na sababu kwa kuandika barua ya kushiriki uchaguzi wa marudio ambao Chama kilishapeleka barua rasmi tarehe 09 Februari,2016 ya kutoshiriki uchaguzi hiuo.

Kwa kitendo chao hicho na kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na maadili ya chama Kamati maalum ya Zanzibar imewasimamisha rasmi uanachama kwa mujibu wa katiba ya ACT Ibara ya 11 (2) kuanzia leo tarehe 19 Februri,2016 kwa ukiukwaji mkubwa wa katiba Ibara ya 7(3)(5)(9),ibara ya 10 (2)(c)(d),Ibara ya 22(1)(2)(4).

Kwa mujibu wa Katiba ya ACT Wazalendo masuala yote ya kinadhamu kwa viongozi na wanachama yanashughulikiwa na Kamati za uadilifu za ngazi husika na kwa kuwa kwa sasa Kamati hizo hazijaundwa Kamati ya Uongozi ya Taifa ndio inayoshughulikia na mambo yote ya kinidhamu.

Hivyo jambo hili linawasilishwa mbele ya Kamati ya Uongozi ya Taifa kwa hatua zaidi na kwa taarifa zaidi naambatanisha na tamko la Chama katika kikao cha tarehe 13 Februari,2016 kilichofanyika Dar es Salaam.

Imetolewa leo tarehe 20 Februari, 2016

Juma Said Sanani
Naibu Katibu Mkuu
Zanzibar
 
CCM mdaini haraka sh 200m huyo mgombea wa ACT -Wazalendo kabla hajazifanyia manuva hizo pesa alizopelekewa na Issa Mbarouk Numbi kutoka CCM Kisiwandui kwa mzee Iddi Seif ili atangaze kushiriki uchaguzi wa marudio.

Kama mnataka chama cha kuwasindikiza si mniruhusu mimi ni mwenyekiti wa chama cha Wakurya Waishio Kilwa Kivinje nije kushiriki, mradi tu mnikingie kifua kuwa chama hiki ni chama cha siasa, kweli CCM mtashindwa na hilo jambo dogo?
Hiyo pesa ya ACT-Wazalendo tupeni achaneni na hao ACT wameshiba.
 
Hiki chama kule Zanzibar kilipata kura hata urais ambazo hazitoshi hata kushinda kiti cha udiwani. Lakini wamo tu kutengeneza headlines
 
Safi sana ACT, lazima muwe na msimamo thabiti na siyo kuyumbayumba...maslahi ya wananchi mbele kwanza!
 
CCM itafanya kila mbinu kuhalalisha haramu yao. Uchafu wa Jecha hautakasiki hata ukioshwa kwa damu ya kondoo.
 
kwa hali hii ni dhahiri kuwa hiyo siku ya uchaguzi ccm watakuwa kama wanachagua viongozi wao wa chama vilee
 
Back
Top Bottom