ACT watakuwa wasaliti wakimuunga mkono LOWASSA

ACT watakuwa wasaliti wakimuunga mkono LOWASSA

hongoli

Member
Joined
Apr 11, 2011
Posts
18
Reaction score
15
Nasikia ACT Wazalendo wanajipanga kutoa tamko la kumuunga mkono Lowassa kwenye urais. Hivyo wao hawatasimamisha mgombea urais, japo hawatakuwa ndani ya UKAWA.

Tamko lao watalitoa tarehe 13-Aug-2015 kwenye mkutano wao mkuu. Itakuwa siku 2 tu kabla ya kuanza kampeni.

Iwapo ACT watamuunga mkono Lowassa watadhihilisha usaliti kwa wazalendo wanaowanga mkono.

ACT ndio chama cha siasa pekee kilichobaki ambacho bado kina uwezo wa kubeba mamlaka ya kukekemea ufisadi tofauti na vyama na CHADEMA au vyama vingine vya UKAWA ambavyo vimeishapoteza uelekeo.

Wakimuunga mkono Lowassa hawatakuwa na tofauti na vyama vingine vilivyokana ufisadi wa CCM.

Wasiposimamisha mgombea urais, chama kitakosa fursa ya kujijenga. Kitapoteza nafasi ya msingi hata ya kupata ruzuku ya kuendesha chama.

Kisiposimamisha mgombea rais, kitapata wabunge na madiwani wachache sana maana kitakuwa sio chama cha kushika dola. Wananchi wengi huchagua wabunge ili kumsaidia mgombea urais kama atashinda uchaguzi.

Hakuna chama nchini ambacho kimewahi kupata wabunge na udiwani kwa kutosimamisha mgombea urais. CHADEMA wanakumbuka makosa kama hayo waliyafanya kabla ya mwaka 2005.

Uhai na kifo cha ACT Wazalendo utategemea tamko lao la 13-Aug-2015

ACT wakimuunga mkono Lowassa watapoteza umaana wa azimio lao la Tabora.

ACT wakimuunga mkono Lowassa itajulikana ni kweli kwamba yeye ndio aliyekuwa anaki-fund na kusaidia kuanzishwa kwake.
 
Back
Top Bottom