GE2025 ACT Wanatuambia Linda kura! Na sisi tunasema Linda Kura’ Bila Reforms ni Utapeli wa Kisiasa na Usaliti kwa Demokrasia ya Taifa Letu

GE2025 ACT Wanatuambia Linda kura! Na sisi tunasema Linda Kura’ Bila Reforms ni Utapeli wa Kisiasa na Usaliti kwa Demokrasia ya Taifa Letu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
519
Reaction score
1,463
Katika wakati ambapo wananchi walioamka wanapaza sauti kwa umoja na msimamo thabiti wakisema NO REFORMS NO ELECTION – yaani bila mabadiliko ya kweli ya mfumo wa uchaguzi hakuna sababu ya kushiriki uchaguzi wa maigizo – chama cha ACT-Wazalendo kinakuja na kauli isiyokubalika ya "Linda kura".

Swali la msingi ni hili: unalinda nini kwenye mfumo wa kisiasa uliojengwa juu ya udanganyifu, uonevu, na ukandamizaji wa demokrasia?

Unalinda kura zipi ambazo hata kabla hazijapigwa tayari zimeandaliwa kuibiwa kupitia tume isiyo huru, daftari lililochakachuliwa, na sheria kandamizi zisizotoa haki sawa kwa vyama vyote?

ACT-Wazalendo, kwa kauli zao hizi, wanazidi kujidhihirisha kuwa si chombo cha ukombozi wa kisiasa bali ni "controlled opposition" – chama kidogo kinachoishi kwa makombo ya mfumo wa CCM kwa kisingizio cha realism. Huu ni usaliti wa kisiasa kwa wananchi wanaotafuta mabadiliko ya kweli.

Katika mazingira ambapo uchaguzi ni predetermined, tume ya uchaguzi ni state-captured, na vyombo vya dola ni biased tools of repression, hoja ya "Linda kura" ni kichekesho cha kisiasa kilichojaa political naivety au complicit intent. Ni sawa na mtu anayelinda mzoga ukifikiri bado una uhai.

Wananchi wanaelewa, na historia inashuhudia: hakuna mabadiliko yanayopatikana kwa kulinda udanganyifu. Mabadiliko ya kweli huanzia kwenye kusimama kidete na kudai REFORMS kabla ya chaguzi yoyote kufanyika.

Kwa hiyo tunarudia kwa msisitizo:
NO REFORMS, NO ELECTION.
Sio Linda Kura bali Linda Demokrasia kwanza.
ACT-Wazalendo wasituchanganye na siasa za kulinda maslahi yao ya kisiasa kwa mgongo wa wananchi w
aliodhulumiwa.
 
Sure, walikuwa wapi kulinda 2019, 2020 na 2024?

..Zanzibar kura zinapigwa siku mbili.

..Siku ya kwanza wanapiga Polisi, Jeshi, na watumishi wa Tume.

..Siku ya pili ndio wanapiga wananchi wote.

..Sasa unajiuliza kuna ulazima gani kuwa na utaratibu huo?

..Mbona Tanganyika tuna wapiga kura wengi zaidi ya Zanzibar na kura inapigwa kwa wakati mmoja?

..Pamoja na mauzauza hayo ACT wameona haina haja ya kugomea uchaguzi mpaka mabadiliko yafanyike.
 
Nakumbuka last time tulijipanga kulinda kura zetu, haa😳, majamaa yakatangaza kwamba piga kura rudi nyumbani, vinginevyo tusilaumiane😀😀😀, waliojichanganya kweli walikula virungu.
So ni bora tu kudai reforms. Na kama hakuna reforms bora kuendelea na majukumu yangu kuliko kwenda kupoteza muda kupanga mstari wakati matokeo wanayo.
Na wangepunguza gharama za kufanya uchaguzi pesa hizo wakafanyia mambo ya maana mahospitalini na mashuleni
 
..Zanzibar kura zinapigwa siku mbili.

..Siku ya kwanza wanapiga Polisi, Jeshi, na watumishi wa Tume.

..Siku ya pili ndio wanapiga wananchi wote.

..Sasa unajiuliza kuna ulazima gani kuwa na utaratibu huo?

..Mbona Tanganyika tuna wapiga kura wengi zaidi ya Zanzibar na kura inapigwa kwa wakati mmoja?

..Pamoja na mauzauza hayo ACT wameona haina haja ya kugomea uchaguzi mpaka mabadiliko yafanyike.

Hata wakigoma CCM hawawezi fanya mabadiliko
 
Back
Top Bottom