ACT-Tanzania wajitosa sakata la CUF

ACT-Tanzania wajitosa sakata la CUF

Hiki chama si ni Tawi la CCM?

Wanalaani ama wamefurahishwa?
 
ACT Ipi inayotoa taarifa hii? Ni ACT waasisi au ACT masalia
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI,

CHAMA cha Alliance For Change and Transparance( ACT- Tanzania.)kiki zingatia msingi wa utu na uzalendo kwa taifa,kime pokea kwa masikitiko tukio la kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF),Prof.Ibrahim Lipumba huko mtoni Mtongani Katika Wilaya ya Temeke. jijini Dar esSalaam jana.

Msingi wa kukamatwa Prof Lipumba na wenzake ni kwa ajili ya kuadhimisha kumbu kumbu ya mauaji ya Watanzania Wenzetu yaliyofanywa na jeshi la Polisi miaka 14 iliyopita wakati watanzania hao wasio na hatia walipotumia haki yao ya kidemokrasia kufikisha ujumbe kwa serikali kwa njia ya maandamano.

Kama iliyokuwa miaka 14 iliyopita kwa jeshi la Polisi kushindwa kutumia weledi wa kazi yao na kujiepusha na mihemko ya kisiasa jana tena wameendeleza uoneu wao kwa watanzania katika jitihada za kuminya Demokrasia na kufikisha mawazo huru kwa watawala wetu kwa kisingizio cha uwepo wa tishio la Ugaidi.

Kwa kutumia hoja dhaifu na visingizio vilivyo jaa mihemko ya kisiasa jeshi la Polisi likajiingiza katika kuwakamata na kuwadhalilisha viongozi wa (CUF), lengo likiwa ni kuwatisha watanzania hasa wakati huu tunapoelekea katika uchaguzi mkuu wa Rais Madiwani na wabunge.

Sisi ACT-Tanzania tunaofuata misingi ya haki na uwajibikaji tunalaani vikali matendo ya jeshi la polisi kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa kukabiliana na viongozi wa kisiasa kama ilivyofanyika jana.

Aina hii ya nguvu ya jeshi la Polisi kwa ajili ya kukilinda chama kilicho madarakani ndiyo iliyopelekea kuuawa kwa mwanahabari Daudi Mwangosi miaka miatatu iliyopita jambao ambalo hatupendi lijirejee kwa mtanzania Mwingine.

Tunalitaka jeshi la Polisi litende haki kwa vyama vyote kwa kuacha uwanja huru wa kufanya siasa, hasa tukizingatia wakati huu wanapowazuia viongozi wa CUF na kuwaruhusu wa CCM kufanya mikutano sehemu mbali mbali nchini kwa njia ya maandamano.

Mwisho tunatoa Pole kwa Prof.Lipumba wanachama n viongozi wote wa Cuf waliokamatwa hapo jana.

ACT TANZANIA TAIFA KWANZA
Imetolewa
Na Mohmmed Massaga
NAIBU KATIBU MKUU BARA
+255 718 388 888
Tarehe 28/01/2015.

Tuondoleeni unafiki wenu. Mnatafuta pa kutokea! Wapuuzi sana nyie
 
Tatizo tamko hili halijabainisha bayana kuwa hili ni tamko la ACT Nyankurungu au ACT Dotto Rangimoto.

All in all, tunashukuru kwa tamko lilienda shule sio kama yale ya siku zote, Pia endeleni kutoa matamko kama haya yenye akili huenda umma ukawaamini.

#GOODMORNING .
 
Ah hawa jamaa wameamua kutumia barabara ambayo hairuhusiwi (no entry) shauri yao watakamatwa bure na traffic police
 
ACT-TANZANIA ni chama cha siasa kinachojipambanua na vyama vingine ambacho kimekuja na hakitaki kufanya siasa za mazoea hichi ndio chama pekee kikichoamua kuwasemea watanzania bila kubagua suala hili linamuhusu nani
 
hili nia tamko rasmi la chama pia ACT-Tanzania kwa muda mchache sana imeaminika kwa umma ndio maana wamwamua kutupa viti vya uenyekiti wa mitaa tofauti na vyama vingine wamekuja kuaminika baada ya miaka 10
 
hili nia tamko rasmi la chama pia ACT-Tanzania kwa muda mchache sana imeaminika kwa umma ndio maana wamwamua kutupa viti vya uenyekiti wa mitaa tofauti na vyama vingine wamekuja kuaminika baada ya miaka 10
 
Hawajitambui hakuna wanachofanya hawa chadema b.
 
ACT mmeonyesha uzalendo sana. Sijasikia Chadema wakilaani hili tukio

unapiga viroba nim hapo sakina bar?
cdm ilituma wakili amtoe lipumba polisi by the.way.ccm.kwanini mnawatumia police kama lady pepeta
 
Back
Top Bottom