ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 643
- 1,603
Hebu tuambie itkadi ya ACT ni ipi?Na pia kwa faida ya Wana JF tuambie wewe ni mwanachama wa chama gani?ACT Ni chama cha kisasa zaidi..kinaendesha mambo yake kidigitali...chama makini cha ACT NI MKOMBOZI WA MTANZANIA
mkuu wakati fulani ni bora ukasoma na kupita kama guest, kama wanavyofanya wageni wenzako! au wewe mwenyeji? lakini sasa kama wewe mwenyeji mbona unakuwa hivyo?Ache uhuni
mkuu wewe unaijua itikadi ya ACT-Tanzania, maana hatari iliyopo ni kwamba kama utakuwa unamuuliza mwenzako wakati nawe hujui, hata ikitokea ukidanganywa; itakuwa ni vigumu kugundua.Kama wewe tayari unaelewa jibu la swali ulilouliza, basi hamna shida kaka!Hebu tuambie itkadi ya ACT ni ipi?Na pia kwa faida ya Wana JF tuambie wewe ni mwanachama wa chama gani?
kweli kabisa ndugu, usiwape namba yako kabisa maana ukiwapa namba yako ya simu watakuibia simu yako, halafu ukiwapa parua pepe watakuibia E-mail yako. Yaani ni hatari sana! usikubali kabisa mkuu!waizi tu siibiwi tena.
Mkuu, mtu yeyote mwenye akili anapokutana na mtu mshari, humjibu kwa salama! mara nyingi mtu mwenye hekima hapayuki payuki bali huongea kauli thabiti kwa sauti ya chini na yenye utulivu mkubwa lakini huwa mara nyingi inakuwa nzito (kama anayezungumza ni mwanaume). Basi hapo utakuta watu wote kimyaaa! ni hivyo tu mkuu, kwa kawaida haki inaposimaa batili hujitenga kwa kuwa haki na batili daima hazichangamani.je! ni kwa vipi tunaweza kumtofautisha yule anayejua jambo dhidi ya yule asiyefahamu jambo?Asante comred kwa hizi taarifa njema kuna wahuni watakuja hapa lakini sisi tuwajibu kwa adabu.
Mtu mwenye akili ni yule ambaye pale anapokuwa hafahamu jambo lakini apatapo kufahamishwa, huelewa na akakifanyia kazi kile alichokielewa ikiwa ni pamoja na kuwaelewesha wengine, lakini mtu mjinga, ni yule asiyejua kitu ila hata anapofahamishwa kitu haelewi wala hana nia ya kuelewa, lakini ataelewaje na wakati hajui, na hajui kwamba hajui!?Hiki chama mlichemka mlipoanza kujenga msingi wa uhalali wenu kwa ku-attack Chadema.
Kila ajaye kwa shari,riziki magembe amepewa kazi ya kuichafua act mitandaoni...unajisumbua tu utashindana lakini utashindwa
Ndugu watanzania wote, tunawasalimu kwa salamu inayoashiria mabadiliko na uwazi.
Katika kusimamia dhana ya uwazi na kuhakikisha kwamba kila anayependa kupata taarifa mbali mbali kuhusu chama cha ACT-Tanzania, anazipata kikamilifu, kwa haraka, kwa ufanisi na bila usumbufu mkubwa, tunawaomba watanzania wote wanaopenda kupata taarifa mbali mbali za chama cha ACT- Tanzania, watutumie barua pepe zao au namba zao za simu.
ACT-Tanzania tunatumia na tutaendelea kutumia mbinu mbali mbali ili kujitahidi kuwafikia watanzania wengi iwezekanavyo (ikiwezekana wat u wazima wote na wenye akili timamu), kwa haraka, kwa ufanisi, bila usumbufu mkubwa na kwa kujaribu kutumia njia ambazo ni za gharama nafuu zaidi.
Miongoni mwa mbinu ambazo baadhi tumeanza kuzitumia na tutakuwa tunazitumia kuwafikia watanzania ukiacha mikutano ya hadhara, ni pamoja na hii ya kupitia simu zenu, barua pepe zenu, tovuti ambayo tutaifungua karibuni, vitabu, vipeperushi (brochures), mitandao ya kijamii na kadhalika.Tutakuwa tukiboresha mifumo yetu ya mawasiliano kila mara kulingana na uwezo wetu ili watanzania waweze kuyafaidi matunda ya chama chao wakati wote.
NB. Kwa sasa kuna vijitabu vidogo (Brochures) tunagawa vinavyoeleza mambo muhimu yanayohusiana na ACT-Tanzania kwa muhtasari.Kama mtu anahitaji "soft copy", atatutumia e-mail yake na kama anataka "Hard Copy" atasubiria kidogo hadi tutakapoingia mtaani kwake.
ACT-Tanzania.................Taifa kwanza leo na kesho!,
Mabadiliko na Uwazi.........Chukua Hatua!.
Tuwasiliane kwa acttanzania@yahoo.com au acttanzania@gmail.com.
Mimi sio mtaalamu sana wa mambo ya uhasibu lakini nilishawahi kuambiwa na mtaalam mmoja wa mambo ya fedha kwamba mara nyingi taarifa za mapato na matamizi ya taasisi, hutolewa katika vipindi vya robo mwaka, nushu mwaka, robo tatu na mwaka.Sasa sijui kama alichokuwa ameniambia kilikuwa ni ukweli au laa! nadhani wataalam wa mambo ya uhasibu wanaweza kutusaidia ujuzi katika eneo hili, ila kama ilikuwa ni ukweli na kama ACT-Tanzania watakuwa wanafuata utaratibu huo wa kitaalam (kama itakuwa kweli ndivyo unavyotakiwa uwe), basi bila shaka wanaweza wakatoa baada ya kufikisha robo mwaka! pengine tusubiri kidogo halafu tuone kama ACT- Tanzania itafanya hivyo au laa!Tunaomba ACT muishi kadri ya msingi wa UWAZI ambao utawatofautisha na vyama vingine.
Kwa kuanzia wekeni wazi mambo ya pesa zilizogharimia usajili.
Nani walichangia, na kwa kiasi gani, na zilitumikaje.
UWAZI mkiuweka katika matendo mtatupata wanachama wengi.