Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,286
ACT NA KUSHINDWA KWA KAFULILA.
Kumekuwa na uvumi katika mitandao ya kijamii kuwa chama chetu cha ACT kimehusika katika kushindwa kwa David kafulila. Wengine wanaenda mbali zaidi kwa kumhusisha Zitto Z Kabwe katika hili.
Kama chama hakiwezi kujibu kila tuhuma, sababu kama kikianza kujitia kazi kujibu hakitaweza kufanya kazi zake, sababu watu hawaishi kusema na kila siku huibuka jipya.
Hata hivyo, hili mimi binafsi naomba kulijibu, na nina lijibu kama mwanachama tu wa ACT ambaye huona tabu chama chake kuzushiwa mambo yaso kweli na yenye lengo la kukitoa chama katika reli na kukiingiza katika majibizano.
Mosi.
Kama kuweka mgombea katika jimbo la Kigoma Kusini na kufanya siasa katika jimbo hilo ndio kunachukuliwa kuwa ni uhusika wetu katika kushindwa kwa Kafulila, hili linakuwa si sahihi hata kidogo.
Kama chama cha siasa tusingependa chama chochote kishinde Kigoma Kusini tafauti na ACT, na ndio maana tulipeleka chama, tukafanya siasa, tukaweka mgombea na tukafanya kampeni, na kampeni zetu nchi nzima zilijikita katika masuala ya wananchi na taifa lao. Hatukajaribu hata kidogo kujadili mambo kinyume na hivyo.
Kila chama kilikuwa na haki hii katika jimbo lile lakini pia kilikuwa na wajibu huu kwa wanachama wake! Huu huwezi kuuita mpango makhususi wa kumuangusha Kafulila bali ni mpango makhususi wa kushinda jimbo, na kila chama na kila mgombea alikuwa na mpango huu, hata Kafulila alikuwa na mpango huu, na katu hatuwezi kuuita ni hujuma kwetu.
Pili.
Kutochaguliwa tena Kafulila hakujasabishwa na ACT bali kumesababishwa na uhusiano uso ridhisha kati ya Kafulila na wapiga kura wake. Kweli kabisa Kafulila atabaki kuwa mbunge wa kukumbukwa na kwa vyovyote vile pengo lake litaonekana katika bunge hili jipya. Uhusiano wa Kafulila na wapiga kura wake haukuwa mzuri kutokana na sababu zifuatazo.
1. Kafulila amekuwa mbunge wa kitaifa zaidi kuliko kuwa mbunge wa Kigoma Kusini, amejitahidi sana kulisemea taifa juu ufisadi na mambo mengine ya kitaifa.
Wakati akifanya hivyo, jimbo lake lina changamoto nyingi, na wapiga kura walikuwa wanamuhitaji mbunge wao lakini yeye alikuwa na anashughulishwa zaidi na escrow na mambo ya kufananayo. Barabara za jimbo lake ni tatizo, ameshindwa kupambana kushinikiza miradi ya kimaendeleo ifanyike katika jimbo lake kwa wingi.
Wapiga kura walikuwa wanalalamika huku wakitoa mifano jinsi Zitto alivyopambana kuhakikisha Kigoma inaunganishwa na mikoa mingine, hususani ushiriki wake katika ujengwaji wa daraja la Kikwete, daraja ambalo halijafungua fursa kwa Kigoma Kaskazini tu lakini pia kwa Kigoma nzima hata Zitto aonekane mbunge wa Kigoma.
Wakati wakulima na wajasiria mali wa Kigoma Kaskazini wakinufaika na huduma ya hifadhi ya jamii, Kigoma Kusini hicho kitu hakina nguvu na wala hakisisitizwi kama kilivyosisitizwa na Zitto Kigoma Kaskazini.
2. Kitendo cha Kafulila kwenda kumnadi Lowassa Kigoma, mtu ambaye wanaKigoma bado wanamtazama kwa jicho la ufisad pia kumesababisha Kafulila kupotea kama alivyopotea Wenje. Walimuona Kafulila mnafiki na asiyesimamia anacho kiamini, huwezi kumnadi mtu uliyemtukana kwa miaka mitano katika majukwaa ya siasa kwa kusema afaa kuwa rais na bado wenye akili zao wakuelewe.
Naomba mjue, Lowassa baadhi ya mikoa au majimbo alikuwa turufu ya ushindi, lakini katika mikoa na majimbo alikuwa galasa lisilo na madhara mbele ya turufu. Mkoa wa Kigoma na Mwanza ni miongoni mwa mikoa ambayo Lowassa alikuwa galasa lisilo na madhara! Kafulila alikosea sana kwa kumnadi Lowassa na kumshambulia Zitto.
Huwezi kumshambulia Zitto Kigoma kisha wanaKigoma wakuache, mtu ambaye wanamtazama kama alama ya kufunguka Kigoma. Kafulila alimshambulia Zitto jukwaani na katika mitandao ya kijamii lakini pia akampamba Lowassa katika majukwaa, wanaKigoma wakaamua kumkata. Hili sio kosa la ACT bali ni la Kafulila mwenyewe!
3. Kama kuna ugomvi basi si ACT na Kafulila bali wanaKigoma na Kafulila. Kafulila aliwatukana wanaKigoma kuwa wao wanachojua ni kulima mawese na si kuanzisha chama, na hawahitaji chama cha siasa. Sababu kwanini walipoikubali CHADEMA au NCCR hawakuambiwa kuwa si watu kuanzisha chama? Ina maana kwao ni kosa kuikubali ACT? Kwanini chama wanachokikubali Kafulia akiite cha Kigoma ikiwa vyama vyote huwa vya kitaifa? Maswali haya majibu yake yalikuwa ni matusi kwa wanaKIGOMA.
Haya yalionekana ni matusi kwa wanaKigoma kiasi wamzomee akiwa jukwaani. Maneno yale aliyasema Kigoma mjini, lakini yalisambaa haraka Tanzania nzima, na wanaKigoma wakaonesha machungu yao kupitia sanduku la kura.
Hili haliwezi kuwa kosa la ACT, na wanaKigoma na baadhi ya watanzania wanaofurahia kushindwa kwa Kafulila hakuwez kuwa kosa pia la ACT, ingawa pia ni kweli wengi wa wanao shangilia kushindwa kwa Kafulila ni wanaKIGOMA na pia wanaKIGOMA hawa wana vyama vyao, na wapo baadhi ni ACT.
3. Chama kilichopambana kwa kufa na kupona kuhakikisha Kafulila harudi bungeni ni CCM, na kilitumia ofisi ya Wilaya na ya mkurugenzi katika kufanikisha hili, ACT hatukushiriki katika hili na kama chama hatuwezi kufurahia uvunjifu wa sheria katika zoezi la uchaguzi. Kweli pia Kigoma Kusini kulikuwa na viashiria vya wizi wa kura, lakini ni ajabu mtu akianza kuishutumu ACT juu ya hili.
Hata hivyo, kama Kafulila angemzidi wa CCM kwa kura zaidi ya eflu ishirini kwa mfano, hata CCM wangeiba vip wasingeweza kuziba utafauti huo wa kura. Kafulila kapata ushindi mwembamba mno kama alivyoshinda Wenje kwa ushindi huo mwembamba. Ushindi wa kuzidi kura 100 kunatoa mwanya kwa CCM kupiga goli la mkono.
Kama Kafulila angekuwa na adabu kwa wapiga kura na kwa wakigoma wenzake, asingepata ushindi mwembamba, hili ni funzo kubwa sana kwa wabunge walioshinda sasa. Mkichaguliwa kuwa wabunge msiote pembe, cheo dhamana tu!
Nakutakia maisha mema ya kulima mawese.
Njano5
0784845394/762845394