Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,198
- 7,539
ACT nawaasa ndugu zangu,
Msikae mkafikiria kuwa itatokea bahati nasibu tu mara hao...... Mmefikia malengo. La hasha! Hilo haliwezi tokea ndugu zangu. Ni lazima mjilazimishe kufikiri zaidi na zaidi kuona ni namna gani mnaweza kuitekeleza misingi yenu pamoja na kuwa hamkushinda uchaguzi. Mnaweza kukuta hamshindi uchaguzi kwa miaka 100 mfululizo, ina maana hamna mtakachokuwa mnafanya kipindi chote hicho kwa hoja ya kuwa hamjashinda uchaguzi!? Hoja ya kwamba mtakuwa mnaikosoa serikali: tushasema humu mara nyingi kuwa kufanya kazi ya kukosoa wengine " peke yake" ni kujidunisha mno kwani kazi hiyo haihitaji kutumia akili, ubunifu na wala haikuongezei thamani, hivyo ni lazima vyama vya upinzani vifanye zaidi ya hapo ili viwe na thamani inayostahili. Aidha, kama ishu ni kukosoa, tayari kuna mavyama kibao ambayo yanakosoa na pia unaweza kukosoa tu hata kama huna chama na kwa mantiki hiyo ACT inakuwa haina sababu za kuwepo.
Rehasal:
Unapotaka kuwa mtu wa aina fulani, mara kwa mara unatakiwa ujifananishe vile unavyotaka kuwa ili uwe kweli.Kila mara unatakiwa kufanya kila liwezekanalo ili uwe vile utakavyo na usipofanya hivyo usitarajie kuwa. Jiulizeni mna ndoto ya kuwa vipi!? Ni misingi na njia gani zitawafikisha huko!? Kisha mu practice kuanzia sasa na wala si kesho achilia mbali mambo ya habari za eti mpaka tutakaposhinda uchaguzi.
Misingi
Mlituambia mna misingi kumi (10)isn't it?. Kati ya hiyo ni kutetea na kulinda utu na mwingine ni kuhakikisha kila mtu anakuwa na hifadhi ya jamii. Kwa hakika misingi hii miwili tu inawapa kazi ya kufanya kwa saa 24 kuanzia sasa na ni kazi nzito inayoweza kuibadili Tanzania.
Kwa kuwa watu wanaofanya kazi kwenye mifumo rasmi wana hifadhi ya jamii rasmi kwa mujibu wa sheria, hao mnaweza kuachana nao. Kwa wale wenye nguvu na akili timamu, wanaweza kufanya kazi na kujiwekea akiba kupitia voluntary schemes na wakaishi maisha yenye heshma uzeeni, achaneni nao.By the way mnaweza kushughulika nao baadae.
Ndugu zangu: kuna wazee dhoofu l' hali na walemavu ambao hawana uwezo wa kufanya kazi yeyote na amma hawana ndugu, au ndugu zao wamewatalekeza.Kundi hili linaomba omba mitaani na kulala chini ya miti. Ukipita mabarabarani utawaona wamelala mitaroni wanapigwa na vumbi na kila aina ya shuruba na kudhalilika kana kwamba si binadamu wenzetu. Kundi hili limetelekezwa bila msaada wowote na watu hawa si kwamba wanafanya makusudi, hanawana uwezo wa kujikimu wala kufanya kazi lakini bado wana uhai.
Ndugu zangu: wasaidieni watu hawa. Narudia, wasaidieni watu hawa kama sehemu ya utekelezaji wa msingi wenu wa utu na hifadhi ya jamii. Amin nawaambia kweli: ikiwa mtafanya hivyo, hata kama hamtashinda uchaguzi milele, malipo yenu mtayapata hapa hapa duniani na kwa Mungu mtakuwa na malipo makubwa. Mtakuwa mmetoa mchango azizi kwa jamii ya mwanadamu: watanzania wenzenu na mwisho wa yote mtakuwa mmetekeleza misingi yenu bila hata kuwa madarakani. Hayo yatakuwa ni mafanikio makubwa na ushindi adhwimu kuliko hata kushinda uchaguzi mkuu. Hili litawafanya muweze kufanikiwa bila kuzozana, kuwa na maadui wasiokuwa wa lazima na kutodhulumu mtu na hali hiyo itawafanya muwe "happy" Ukizingatia kuwa jambo la msingi kupita yote kwa mwanadamu ni kuwa na furaha, mtakuwa mmefanikiwa kulifikia lengo hilo.
Fedha.
Mtu anaweza kusema, sasa fedha zitatoka wapi!? Iko hivi, vyama vya siasa vinapata fedha zinazotokana na michango inayopatikana kwa namna mbali mbali kama vile ruzuku, michango ya uanachama, kujitolea n.k.
Ieleweke kuwa, kuna watu wengi sana duniani ambao wanatamani sana kuchangia kuwezesha wenye shida ila wanashindwa kufanya hivyo kwa sababu kuu mbili. Mosi kukosekana kwa uaminifu, hivyo kushindwa kujua nani tapeli nani mwenye shida kweli na pili, ni kukosekana kwa mipango madhubuti "Strategic Arrangements " ambayo itawezesha misaada hiyo kuleta matunda endelevu. (ntafafanua baadae).
Nini cha kufanya:
Ndugu zangu, tafuteni wataalam wawaandalie mkakati wa namna ya kusaidia hawa watu kwani mtakuwa mnatekeleza msingi wenu wa utu na hifadhi ya jamii kimatendo bila hata ya kuwa serikalini na kuwafanya binadamu wenzenu nao waishi maisha ya heshma. Mpango huo uoneshe lengo, wajibu wa chama, chanzo cha fedha, usimamizi na ufuatiliaji na mambo mengine. Nawahakikishia mtakuwa mmefanya jambo jema na kubwa mno na Mungu atawasaidia.
Kuhusu fedha msijali, mkiwa committed na smart mtapata fedha za kutosha kabisa kutoka kwa binadamu wenye mioyo ya utu. Wa kwanza kuchangia ni mimi ambapo nitatoa Tsh.1000 kila mwezi.
Kwa idhini yenu naomba kutoa hoja sasa.
usitembee juu ya ardhi kwa majivuno